Wabunge Waliamsha Bungeni Sakala la Umeme Kukatika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



SAKATA la uhaba wa umeme limeteka mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa 2023, baada ya wabunge kupaza sauti zao wakiitaka Serikali kuchukua hatua za kutafuta mwarobaini wake, huku baadhi yao wakiitaka iwashirikishe wawekezaji wa sekta binafsi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mjadala huo umeibuka leo tarehe 6 Februari 2024, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, David Mathayo, kuwasilisha taarifa hiyo bungeni jijini Dodoma.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Kilumbe Shaban Ng’enda, ameishauri Serikali ikaribishe sekta binafsi katika kuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji umeme kwa kuwa ina gharama kubwa ndio maana kuna upungufu wa nishati hiyo.

“Kuhusu suala la umeme, gharama ya uzalishaji umeme ni kubwa sana na hasa miundombinu ya uzalishaji. Leo tunakwenda kukamilisha bwawa lililojengwa kwa zaidi ya Sh. 6 trilioni zimetumika ikiwa karibu ya asilimia 18 ya bajeti nzima ya nchi,” amesema Ng’enda na kuongeza:

“Ninachokusudia kusema Serikali isijibebeshe mzigo mkubwa wa kuendelea kuanzisha miradi, ikaribishe sekta binafsi ili iweke mifumo kuhakikisha wanazalisha umeme kwa njia ya ubia au mikabata, wazalishe kisha TANESCO ununue na kuwapa huduma wananchi.”

Kwa upande wake Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma), ameishauri “TANESCO kufanyiwe maboresho na muwekeze kwenye ile miradi ya mifano. Vile vituo muwape sekta binafsi wafanye biashara, sekta binafsi zimeunfwa kwa ajili ya biashara nyie hamtaweza.”

Mbunge Viti Maalum, Ridhiki Lurida, amedai tatizo la uhaba wa umeme linasababishwa na baadhi ya watu wanaohujumu miradi ya uzalishaji umeme kwa maslahi yao binafsi na kuitaka Serikali kuwachukulia hatua.

Amedai kuna baadhi ya watu wanafanya njama za kuukwamisha mradi wa kujenga bwawa la kufua umeme la Mwalimu Julius Nyerere, liliko wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani, ili nishati hiyo isizalishwe kwa ajili ya kupata fursa ya kufanya biashara za kuuza majenera.


“Kuna watu wanachepusha maji hali hii siyo ya kuiachia, nimetembea kutoka Lindi mpaka Dar es Salaam, Daraja la Mkapa katika bonde kuna tuta la mchanga hakuna maji yanayokwenda Mafia, hii athari ni kubwa watu wanacheza na mifumo ya maji Bwawa la Mwalimu Nyerere halitafanya kazi itakuwa historia na kuna watu wameapa halitofanya kazi,” amesema Lurida.

Sakata la umeme limekuwa pasua kichwa tangu mwishoni mwa 2023, ambapo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, aliagiza hatua madhubuti zichukuliwe ili kuondoa athari zake hususan mgawo wa umeme.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad