Alikiba Azindua Radio yake, Awapiga Dongo Wasafi Media

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Alikiba Azindua Radio yake, Awapiga Dongo Wasafi Media

Supastaa wa Bongo Flava, Alikiba amezindua kituo cha redio kwa jina “Crown FM”. Uzinduzi huo ulifanyika usiku wa Jumamosi Machi 9 2024 katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dare es Salaam kwenye sherehe ya miaka 20 ya Kiba katika muziki.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, Kiba alielezea kwamba vyombo vya habari ni muhimu ndivyo vimemkuza kama mwanamuziki na anakumbuka alizawadiwa redio ndogo na babake wakati akikua.


Mwimbaji huyo alisema pia kwamba changamoto ambazo amepitia pia zilimpa msukumo wa kuanzisha kampuni ya uanahabari ambayo ina kituo cha redio na cha runinga.


Crown FM ambayo itapeperusha matangazo yake kwenye masafa ya 92.1 FM inapatikana jijini Dar es salaam, kisiwani Zanzibar, Tanga pamoja na eneo la Pwani nchini Tanzania.


Sherehe ya miaka 20 ya Ali Kiba ilihudhuriwa na viongozi wengi mashuhuri nchini Tanzania akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Nape Nauye Waziri Wa Habari,Mawasiliano Na Tecknolojia Ya Habari, Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwigulu Chemba ambaye ni Waziri wa Fedha na Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Chalinze.


Wanamuziki wenza walikuwepo pamoja na wajasiriamali mbali mbali nchini Tanzania.


Baada ya uzinduzi wa Radio yake kwa jina #CrownFm akiwa jukwaani wakati akiimba, Kiba amesema kuwa “Hii sio media ya familia ambayo watu wengi walioajiriwa ni ndugu.”


Je, unahisi kamaanisha Nini au ujumbe ni wa nani ?


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad