Huyu Hapa Mtoto wa Wastara na Marehemu Sajuki, Atimiza Miaka 12

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Pichani Farheen mtoto wa Wastara na Sajuki asherehekea kutimiza miaka 12. Wastara afunguka yafuatayo....

"Kheri ya kuzaliwa kipenzi changu mtoto wangu wa kike wa pekee shoga yangu, ndugu yangu mpenzi wangu nakupenda sana wewe ni kumbukumbu nzuri sana kwenye safari ya maisha yangu sichoki kukuangalia uso wako unanikumbusha sana siku ya pili baada ya kuzaliwa babaako aliuliza tunampa jina gani binti yetu nilikuwa nimeandaa jina la kukupa hasa kwa wakati tuliokuwa nao baba'ako alikuwa mgonjwa sana nikasema Farheen

Akashindwa kulitamka akauliza nini maana yake hilo jina? nikwambia maana yake furahieni, nikamwambia tumepewa zawadi na Mungu lazima tufurahi. Akajibu jina zuri sana nitaliweza tu sababu ni binti yangu unajua alifanya nini? tulipotoka hospital kurudi nyumbani alisema naomba nifue nguo za binti yangu hata kwa leo

Nilikimbilia chooni nikalia sana na kumwambia kwanini umempa mja wako kitu alichokuomba kwenye wakati kama huu hawezi hata kumbeba binti yake kwa dakika 10 tu anatetemeka nilikufuru siku hiyo Mungu anisamehe tena anisamehe sana, niligundua wewe pekee ndio uliyerudisha tabasamu lake lililopotea kwa mwaka mzima.

Ya kuandika ni mengi na yanaumiza sana kwenye maisha ya kuzaliwa kwako nakuombea Mungu uwe mwenye furaha siku zote heshimu kila mtu kuwa mwaminifu mkweli na uwe unajiamini sana utashinda vita za walimwengu NAKUPENDA SANA FARHEEN KILOWOKO BINTI SAJUKI" ameandika Wastara

Sajuki pia alikuwa ni msanii maarufu wa filamu na walianza mahusiano yao baadaa ya kukutana kikazi katika kazi za filamu, walifunga ndoa. Wote waliwahi kupata ajali ya pikipiki iliyopelekea Wastara kukatwa mguu, muda ulivyopita Sajuki nae alianza kuumwa mwishowe kufariki tarehe 2 January 2012
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad