Kutoka Uside Chick na Kukataliwa LIVE Kwenye Media MPAKA Nyota Tano Begani

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa



Miaka sita imepita. Watu wa mitandao hawaisahau 19 Septemba, 2017. Aibu kwa pisi kali ya Daslama mjini. Jiji lenye joto zaidi Tanzania. Namuongelea Hamisa Mobetto 'Misa', baada ya Mondi Bin Laden kumkana 'laivu' kwenye media kubwa. Lilikuwa pigo kwa Misa, Mama Misa na Team Misa.

Mondi akaendelea kumnanga Pisi Misa. Kwamba yuko radhi kutembea kwa magoti mpaka Afrika Kusini. Kwenda kumuomba msamaha 'The Boss Lady', Zarina Hassan. Hii kauli ikawa kama kisu kikali juu ya mfupa wa Misa na wote waliokuwa nyuma yake.

Hii 'momenti' ni moja ya 'memori' mbaya sana kwa Hamisa. Sidhani kama atakuja kuisahau kwenye maisha yake. Lakini wazungu husema: "What doesn't kill you makes you stronger..." Yaani, "Kisichokuua kinakukomaza..." ndicho kilichotokea kwa Misa.

Mtoto mwenye kiuno mbinuo, alipiga moyo konde. Kisha kwa moyo wa ujasiri akaamua kupiga dili zake. Na hapo akaanza kuimarisha himaya ya biashara zake. Ukubwa wa jina lake ndo ikawa fresh kinoma na siyo kinyonge tena.

'Dilizi' mezani kwake kila siku hazikuisha. Tripu zikawa nyingi kuliko idadi ya ndevu za Morrison. Leo Dubai kesho US. Halikuwa tena jambo la ajabu. Ngozi yake ikaanza kujitenga na vumbi la Tandika, ikaiva badala ya kunawiri. Laiiini kama kichanga.

Mara paap Mobetto huyu hapa tunamuona ana-roll na rapa staa kutoka ardhi ya Jay Z na Beyonce kule kwa Joe Biden. Ndevu nyingi. Vocal kali na flow za hatari. Namuongelea Rick Ross The Boss. What? Swali la mshangao likabaki kwa wanga mjini.

Kurasa kubwa za Mtoni zikaripoti ukaribu wa Pisi Misa na Staa Rozee. Bila kusubiri ushuhuda, nina uhakika Diamond alibaki mdomo wazi. Kabla Mondi hajafunga mdomo wake. Mtaa ukamtangaza rasmi Mobetto kwamba 'ndiye mrembo grade one Bongo kwa sasa'.

Nikiandika sana mwisho nitatia chumvi...
Leo acha tuishie hapa

Times FM
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad