Christina Shusho: Niliolewa nikiwa na miaka 19, nilikuwa mrembo balaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Christina Shusho

Christina Shusho


Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Christina Shusho (46) amesema kuwa aliolewa na mchungaji John Shusho akiwa na umri mdogo wa miaka 19 tu na alikuwa mrembo.


Mkali huyo wa nyimbo za Hapo Mwanzo, Ushirika Na Wewe, Wa Kuabudiwa, Mtetezi Wangu, Shusha Nyavu, Relax, Teta Nao, Bwana Umenichunguza na nyingine nyingi anasema;


"Niliolewa na mtu mmoja lakini nilikuwa nahudumia ndugu wa mume wengine nane, nilikuwa mtumwa, nilikuwa mrembo lakini nilikuwa mjinga kichwani. Nikajiuliza hivi nimeolewa au ni mfanyakazi wa hawa watu? Sasa hivi sina ule uzuri tena lakini kichwani niko smart, najielewa na kujitambua.


"Nimeolewa nikiwa na miaka 19 nilipomaliza kidato cha nne nilikuwa mrembo sana, msinione hivi ni vile nimechoka tu, nilikuwa nikipita hivi wanaume walikuwa macho yote kwangu. Uzuri wangu ulimpa hofu mama yangu alikuwa anawaza huyu mtoto na uzuri huu akikaa hapa si ataharibika.


"Basi akajitokeza mzee Shusho akasema nataka kuoa huyu binti, mama hakutaka maelezo akasema chukuaaa chukuaaa chukuaaa!!! asituharibikie hapa, kwa hiyo niliolewa nikiwa na miaka 19 pekee.


"Nilikuwa mdogo na sikuelewa nini maana ya mapenzi wala sikujua maana ya upendo, naweza sema nililazimishwa kuolewa ili nisibaribike lakini ilikuwa si kwa matakwa yangu," amesema Christina Shusho.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad