Harmonize Afunguka Sababu za Kumsindikiza Hadi Chooni Poshy Qeen

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mwimbaji maarufu wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ameendelea kukiri mapenzi yake mazito kwa mpenzi wake, Poshy Queen huku uhusiano wao ukiendelea kuimarika.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide ameposti video iliyomuonesha akimfuata nyuma mama huyo wa binti mmoja alipokuwa akienda toileti.


Mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Tanzania, Poshy Queen
Chini ya video hiyo, Konde Boy anafichua kuwa kuandamana na mpenzi wake anapokwenda msalani sasa imekuwa jambo la kawaida kwake.
“Msichana mrembo zaidi niliyewahi kumuona duniani..Kumsindikiza toileti ni suala la kawaida sasa!! Simuamini, sijiamini,” Harmonze aliandika chini ya video aliyoposti kwenye mtandao wa Instagram.

Mastaa hao wawili wa Bongo sasa wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miezi kadhaa iliyopita.
Habari kuhusu uchumba wao ziliibuka mapema mwaka huu na kusababisha mijadala mingi na msisimko kwenye mitandao ya kijamii.


Harmonize akiwa katika mapenzi mazito kwa mpenzi wake, Poshy Queen.
Mnamo mwezi Machi, Poshy Queen alionesha mapenzi yake kwa kumwandikia mpenziwe Harmonize ujumbe mtamu alipokuwa akifikisha miaka 30.

Mwanasosholaiti huyo mrembo alitumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kummiminia Konde Boy maneno matamu huku akitafakari hadithi yao ya mapenzi.

“Kwa mpenzi wangu na rafiki yangu wa karibu. Ninaomba kwamba miaka yako ya 30 iwe bora kwako na ufanikiwe kila kitu unachotaka, asante kwa kuniletea mimi na kila mtu karibu nawe furaha na furaha nyingi, NAKUPENDA SANA ADAMU WANGU.
“Kukuona ukiwa na furaha sana leo kunanifanya nijisikie mwenye furaha sana byb. Keep that smile on your face for me, God bless you for us daddy. Happy birthday byb,” Poshy Queen aliandika.
Baada ya kuona ujumbe huo, bosi huyo wa Konde Gang alijibu; “Kila kitu kwako mpenzi…Asante nimebarikiwa kuwa na wewe”

STORI NA SIFAEL PAUL, GPL


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad