Shaffih Dauda : Kibu Denis Aheshimiwe Thamani ya Milioni 600 Kaitengeneza Kwa Jasho lake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kibu kaitengeneza mwenyewe thamani yake hadi hapo ilipo leo, unaposema hana thamani hiyo anayoitaja yeye ni kumkosea heshima. Kibu anaamini thamani yake kwa sasa ni zaidi ya Tsh. 600 milioni, kama klabu itaona hana thamani hiyo itamwacha aondoke.

Kibu Denis ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na juzi tu ametoka kucheza AFCON, amecheza mechi za African Football League na CAF Champions League.

Kuna uwezekano mkubwa akawa na ofa kutoka klabu za mataifa mengine [Misri, Morocco, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu nk], kwa sababu kacheza mashindano ya kimataifa vizuri na kaonekana.

Mfano Pyramids au Wydad ikimtaka Kibu, hawawezi kutoa zaidi ya Tsh. 600 milioni? Kwa hiyo inategemea Kibu ana ofa kutoka timu za mataifa gani lakini maraifa kama Misri, Morocco, Qatar, Saudi Arabia kumpa mchezaji kiasi kikubwa cha pesa wala sio jambo la kushangaza.

Platform ambayo Kibu ameipata akiwa Simba na Taifa Stars ni kubwa, kwa hiyo inawezekana ana ofa nyingi ndani na nje ya nchi lakini ukiwaza Kibu ana ofa ya Simba, Yanga au Azam tu ndio hapo utaona Tsh. 600 milioni ni nyingi sana.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad