Wadudu wa ARUSHA wala kiapo mbele ya Paul Makonda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wadudu wa ARUSHA wala kiapo mbele ya Paul Makonda


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amekutana na vijana zaidi ya 223, wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za sanaa maarufu kama 'Wadudu' na kuwataka kuwa walinzi na mabalozi wazuri wa kutangaza mazuri ya mkoa wao na kutojihusisha na uhalifu kwenye jamii. - Makonda amekutana na vijana hao ofisini kwake mjini Arusha ikiwa ni muendelezo wa kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii katika kuwaeleza maono yake na kuwashirikisha ili kushirikiana na mkoa katika kujiletea maendeleo binafsi na kufanikisha malengo ya mkoa. 

Katika Hatua nyingine,Makonda amewataka vijana hao kutumia vipaji vyao vizuri ili viwasaidie kuingiza kipato, akiwataka kumuheshimisha kama ambavyo ameonesha thamani kwao tofauti na vile ambavyo wengi walifikiri.

 Aidha,Paul Makonda ametumia nafasi hiyo pia kuwataka vijana kumtanguliza Mungu kwenye Maisha yao, kuwa na nidhamu na kuchagua uongozi ili kufanikisha kupatiwa mahitaji ambayo tayari walikwisha kuyawasilisha kwake kwenye kikao cha awali ambacho waliketi pamoja.

Vijana hao zaidi ya 223 wamemuahidi Mkuu wa Mkoa kutekeleza maelekezo na maagizo yake, na kuahidi kumpa ushirikiano kwenye utekelezaji wa maono yake mkoani Arusha.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad