KUMEKUCHA: Eng Hersi Said Amethibitisha Aziz K Bado Haja Sign Mkataba Mpya Yanga

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
KUMEKUCHA: Eng Hersi Said Amethibitisha Aziz K Bado Haja Sign Mkataba Mpya Yanga


RAIS wa klabu ya Yanga Sc Engineer Hersi Said amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz Ki bado hajasaini nyongeza ya mkataba mpya klabuni hapo na kubainisha kuwa mazungumzo bado yanaendelea lakini hakuna kilichokamilika baina ya pande hizo mbili.

Akizungumza na Soccer Laduma, Eng. Hersi amesema klabu ya Yanga ipo kwenye wakati mgumu kumpoteza mchezaji kama Azizi Ki huku akasisitiza kuwa hajamanisha wanakwenda kumpoteza Azizi Ki.

"Unajua tulimsajili kwa mkataba wa miaka miwili na huo mkataba umeisha na hiyo ina maana wanaomtaka wanazungumza naye moja kwa moja. Lakini kwa upande wetu bado tunazungumza naye na hakuna kilichokamilika." --- Eng. Hersi

Eng. Hersi amekiri kuwa Azizi Ki ana ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali zikijumuisha baadhi ya klabu kutoka Afrika Kusini lakini amewatoa hofu Wananchi kuwa klabu hiyo ina uhusiano imara sana na mchezaji na wamelifanyia kazi jambo hili kama viongozi kuhakikisha anabaki.


_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad