Mwalimu Atupwa Jela Miaka 30 kwa Kuingiliwa Kinyume na Maumbile

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Mwalimu Atupwa Jela Miaka 30 kwa Kuingiliwa Kinyume na Maumbile

 

Mwalimu wa kiume aitwaye Ramadhan Said Nanyalika (32) mkazi wa mtaa wa Matogoro, Tandahimba Mjini Mkoani Mtwara ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa, amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.


Taarifa hiyo imetolewa leo July 09,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP, Issa Suleiman, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya doria, misako, oparesheni na mafanikio ya Mahakamani kuanzia June 01, 2024 hadi Jume 3, 2024.


RPC Issa amesema “Mtuhumiwa siku za nyuma alijenga urafiki Shuleni na Mwanafunzi wa kiume wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 19 ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kuanza kumnunulia vitafunwa Shuleni na kisha kumtaka Mwanafunzi huyo amtembelee nyumbani kwake, siku Mwanafunzi huyo alipomtembelea nyumbani, Mwalimu huyo alianza kwa kumuonesha video chafu kupitia simu janja yake (smartphone) na baadaye kumtaka amuingilie kinyume na maumbile”


“Baada ya Mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo alikataa na kusema hawezi kufanya kitendo hicho, ndipo Mwalimu alianza kumtisha kwa kumwambia endapo hatokubali kufanya hivyo atapata adhabu za mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kufukuzwa Shule, kutokana na vitisho hivyo Mwanafunzi huyo alilazimika kutekeleza kitendo hicho pasipo ridhaa yake na akamuingilia Mwalimu wake kinyume na maumbile”


_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad