RC Nawanda Anayedaiwa Kulaiwi aachiwa kwa Dhamana - Video

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

RC Nawanda Anayedaiwa Kulaiwi aachiwa kwa Dhamana - Video

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemuachia kwa dhamana aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda leo Julai 09,2024 baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo na kusomewa shtaka moja la kulawiti.


Dkt. Nawanda amepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Erick Marley na kusomewa shtaka hilo na Waendesha mashtaka wa Serikali, Magreth Mwaseba na Martha Mtiti.


Kwa mujibu wa Mwaseba, Mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.


“Mshtakiwa, Yahaya Nawanda, Mkazi wa Nyamata Wilaya Bariadi Mkoani Simiyu unashtakiwa kwa kosa la kumwingilia kinyume na maumbile kumlawiti Tumsime Ngemela, kosa ulilolitenda June 02, 2024 eneo la maegesho ya magari lililoko Rocky City Mall Wilayani llemela Mkoani Mwanza.”


Mara baada ya kusomewa shtaka hilo, Dkt. Nawanda aliambiwa dhamana ya shtaka lake ipo wazi ambapo amekidhi masharti na kuachiwa kwa dhamana hadi shtaka hilo litakapotajwa tena.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad