Rais Magufuli Awanyooshea Kidole Ma- Video Qeen Wacheza Utupu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Magufuli Awanyooshea Kidole Ma- Video Qeen Wacheza Utupu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka watanzania kukemea vitendo vinavyodhihirisha mmomonyoko wa maadili, ikiwemo mabinti wanaocheza utupu kwenye video za muziki.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Jumuiya ya Wazazi mjini Dodoma, na kusema kwamba huwa anashangazwa kila anapowasha Television kutazama muziki, na kukutana na mabinti wakicheza utupu huku wanaume wakiwa na mavazi ya staha, na kusema kwamba ni aibu kubwa kwa wazazi kuangalia mambo hayo.
“Mimi ni shabiki mzuri wa muziki, kila ukifungulia mziki wanaocheza utupu ni wanawake wanaume hapana., nyinyi kama jumuiya ya wazazi umefika wakati wa kukemea mambo haya, tunawafundisha nini watoto wetu, tunapenda mziki, lakini je, hiyo ndio muziki tunayocheza, tumeingiliwa na mdudu gani, saa nyingine unapoangalia TV na watoto wetu ni aibu kubwa, yanayofanyika pale ni aibu, si kwa sababu sitaki watu wastarehe, kama ni kwenye klabu kavue huko, lakini kwa nini uwavulie hata wasiohitaji kuona uc**? Tena kwa muda usio muafaka?”, amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameendelea kwa kuitaka jumuiya hiyo na watu wote kusimamia maadili, huku akivinyooshea mkono vyombo husika vinavyopaswa kushughulika na masuala ya utamaduni wa Mtanzania.
“Ifike mahali sisi kama watanzania, bila kujali vyama vyetu, tulinde maadili yetu, ninyi kama wazazi, sifahamu kama enzi za akina Fatma Karume au kina Maria Nyerere huo ndio ulikuwa mtindo, lakini nina uhakika enzi zile haikuwa hivyo, lakini vyombo vyetu vya habari, wasimamizi wa maadili haya wako wapi, wizara inayosimamia haya wako wapi, je, TCRA wako wapi, Niwaombe ndugu zangu Jumuiya ya wazazi kuikosoa hata serikali kwenye kusimamia maadili ya Tanzania”, amesema Rais Magufuli.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Daima nitakupenda Magufuli kwa kweli unamuono wa kipekee.Sisi kama wananchi Wakati mwengine tunawashanagaa sana wasaidizi wako kwani mambo kama haya wala si ya kusubiri mpaka muheshimiwa raisi kuyakemea. Ndipo pale tunaposema watu wakubali au wakatae Maghufili ni kiboko. Ni kiongozi wa mfano. Magufuli ni mjenga nchi. Ni kiongozi wa nchi mwenye kujitambua na kuwatambua watu wake. Kwa kweli hili la mabinti wa kitanzania kujiachia utupu wa nyama kwenye mitandao ya kijamii na video za muziki linakera sana tunashukuru sana muheshimiwa raisi kaliona hili. MUNGU akubariki sana Magufuli

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa Raisi Magufuli tunakuunga mkono kwa ukweli uliozumngumza, hawa dada zetu wamepotoka kufikiri kuiga kila wanacho fanya wazungu ni maendeleo na kusahau maadili ya
    utamaduni wetu. Heko Mheshimiwa Raisi

    ReplyDelete

Top Post Ad