USAFI WA JIJI HADI AJE RAIS OBAMA?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kuelekea ujio wa Rais Barack Obama nchini wiki ijayo, Jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo litakuwa mwenyeji wa mgeni huyo na ujumbe wake hivi sasa limo katika hekaheka kubwa za kuandaa mazingira stahiki kwa ugeni huo. Dar es Salaam ni moja ya majiji machafu sana duniani, hivyo kila juhudi zinafanywa na mamlaka husika kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi kabla ya ugeni huo haujawasili.
Sasa sehemu nyingi za barabara zinatengenezwa usiku na mchana kwa kujengwa upya au kuzibwa mashimo, ambayo baadhi yake yalikuwa makubwa mithili ya mahandaki. Katika baadhi ya barabara, mchanga na udongo uliokuwa umezimeza kutokana na kutotunzwa kwa muda mrefu sasa vimeondolewa.
Taka zilizokuwa zimezagaa kila kona sasa zinazolewa kwa kutumia magari ya Jiji na ya wamiliki binafsi. Katika sehemu muhimu za Jiji, madawa ya kuua mbu na wadudu yamenyunyizwa, huku baadhi ya wamiliki wa majengo katika sehemu atakazopita Rais Obama wakilazimika kupaka rangi majengo hayo. Harufu mbaya iliyokuwa imeligubika Jiji kutokana na uchafu sasa imepungua kwa kiasi kikubwa.
Ghafla vijana kutoka vijiweni wamepewa ajira ya muda kufyeka nyasi, kuzibua na kusafisha barabara na mitaro iliyojaa majitaka. Kumbe wanakaa vijiweni sio kwa kutaka, bali kwa kukosa ajira. Polisi nao wameendesha kamatakamata ya vijana wengi inaodai ni vibaka, wavuta bangi na vitendo vingine vya kihalifu, huku lengo kubwa likiwa ni kusafisha mitaa kabla ya ujio wa Rais Obama. Wakati huohuo, Machinga wameondolewa katika sehemu atakazopita mgeni huyo na ujumbe wake na vibanda vyao vimefyekwa na tingatinga za Jiji, huku wananchi waishio mikoani wakitahadharishwa kutokuja Dar es Salaam wakati Rais Obama atakapokuwa jijini.
Jiji la Dar es Salaam zinazoendelea hivi sasa jijini kuelekea ujio wa ugeni wa Rais huyo wa Marekani. Tumefanya hivyo kwa sababu mbili kubwa. Kwanza ni kuonyesha kwamba Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu vinao uwezo mkubwa wa kulifanya jiji hilo kuwa safi wakati wote. Pili ni kuonyesha jinsi tunavyojidhalilisha kama taifa kwa kuishi katika mazingira machafu, lakini tunachukua hatua za zimamoto na kukimbizana kufanya usafi tunapoona wageni wanatembelea nchi yetu.
Ni aibu iliyoje kwa Watanzania kuishi katika mazingira machafu tukisubiri wageni waje ndio tufanye usafi. Ni dharau na matusi ya viongozi wetu kwa wananchi, kwamba watu muhimu na ambao wanastahili kuwekwa katika mazingira mazuri ni wageni. Wananchi wanasakamwa walipe kodi na wanafanya hivyo. Pamoja na kulipa kodi hizo, mamlaka husika hazioni umuhimu wa kuwatengenezea wananchi mazingira mazuri kwa kuzoa taka, kutengeneza barabara, kufyeka nyasi, kunyunyizia dawa katika mazalio ya mbu na kadhalika.
Usafi wa mazingira na wa kila mwananchi ni muhimu mno katika ustawi na maendeleo ya binadamu. Wakati kila mwananchi analo jukumu la kutunza usafi kwa nafsi yake na mazingira yaliyomzunguka, mamlaka husika zinapaswa kuwawezesha wananchi kufanya hivyo. Inawezekanaje halmashauri za miji na wilaya, kwa mfano, zishindwe kuweka magari ya kuzoa taka kutoka barabarani na mitaani? Zipo wapi dampo za kumwaga maelfu ya tani za taka zinazozalishwa katika makazi ya watu mijini kila siku?

Source:Mwananchi
 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad