MKANDA WA UCHOCHEZI WA SHEIKH PONDA WANASWA NA SEREKALI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

*Arekodiwa akihamasisha Waislamu kuasi
*Amtumia Mtume kupinga uteuzi wa Rais
SERIKALI imenasa kanda za video zinazomuonyesha Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, akitoa mahubiri yanayowahamasisha waumini wa dini ya Kiislamu kuanzisha uasi dhidi ya serikali.

Tukio la kunaswa kwa kanda hizo limekuja ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Polisi Zanzibar kutangaza kumsaka Sheikh Ponda kwa tuhuma za uchochezi, akingali anatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Dar es Salaam kumkuta na hatia ya kosa la uchochezi.

Katika kanda hizo ambazo MTANZANIA Jumapili imefanikiwa kuziona, Sheikh Ponda, amerekodiwa akiwa katika Msikiti wa Mbuyuni, Zanzibar, alikohudhuria Mhadhara wa Dini ya Kiislamu, akiwataka waumini wa dini hiyo kuchukua hatua za kuikomboa Zanzibar kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kutoka kwenye mikono ya utawala wa makafiri.


Huku akiitikiwa kwa neno Takbir kutoka washiriki wa mhadhara huo, Sheikh Ponda anasikika akisema Zanzibar ni nchi ya Kiislamu, hivyo Waislamu wana wajibu kwa kuikomboa kutoka mikononi mwa vibaraka wanaoiongoza, aliodai kuwa wananyonya uchumi wake na kuutoroshea nje ya visiwa hivyo.

Moja ya kanda hizo iliyorekodiwa kwa muda wa saa moja na dakika ishirini na nne, ambayo Sheikh Ponda alitumia muda mwingi kusisitiza umuhimu wa Waislamu kuikomboa Zanzibar kutoka mikononi mwa aliowaita makafiri, anasikika akisema:

“Mna wajibu wa kuikomboa Zanzibar na si mnaweka vibaraka, wanateuliwa huko halafu wanakuja hapa kuwaongozeni, fedha zote zinachukuliwa hapa na kupelekwa kule kwa sababu tumepoteza nchi, tumepoteza hadhi. 

“Makafiri wanatakiwa kuyaheshimu mambo matakatifu ya Kiislamu na kuyajua, kama hawataheshimu Mwenyezi Mungu alisema lazima mlipize kisasi katika mambo matakatifu. Mungu alisema ni lazima mlipize kisasi mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Mambo matakatifu yamewekewa kisasi. 

“Miongoni mwa mambo matakatifu yaliyowekewa kisasi ni haki na uadilifu pamoja na dini ya Kiislamu, unapozungumzia dini ni pamoja na masheikh, hawa ni watu watakatifu, watu wenye hadhi, ni watu wakubwa na watakatifu kuliko baba mtakatifu kama wanavyosema wao.”

Sheikh Ponda pia anasikika akieleza kuwa Waislamu wamedhalilishwa kwa muda mrefu, hivyo wana wajibu wa kuikomboa Zanzibar kwa kuwa hata Mtume Mohammad aliongoza jeshi akakomboa nchi ya Maka kipindi cha Mwezi Ramadhani.

Alieleza kushangazwa na uteuzi wa Rais wa Zanzibar kufanyikia Dodoma na hata uamuzi wa kumuondoa madarakani kuchukulia mkoani humo na kutoa mwito wa jambo hilo kusitishwa.

Katika hili anasikika akisisitiza kuwa; “Hakuna mtu ambaye haelewi kwamba Zanzibar ipo mikononi mwa watu wasio stahiki, Zanzibar ni nchi ya Waislamu. Sisi Waislamu wa Zanzibar tuna mazingatio makubwa kuliko watu wengine kipindi hiki cha Mwezi Ramadhani kwa sababu mafundisho tunayoyapata katika maisha ya Mtume Mohammad ni sawa na mazingira ya sasa, hivyo tunatakiwa kuyatekeleza. Zanzibar si nchi ya watu, bali ni ya Waislamu.

Katika mahuburi yake kwenye mhadhara huo, Sheikh Ponda anakisika akieleza kuwa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika umezaa ufisadi visiwani humo na kurejea kauli aliyodai kutolewa na Mtume iliyokuwa ikiwaonya Wazanzibari kutoruhusu uwepo wa Muungano.

“Tangu lini bia, ukahaba ukawa hitajio la Wazanzibari na hii ndiyo ‘product’ iliyotokana na Muungano na Mapinduzi. Maovu ambayo hamkuyapata kuyaona ni kauli ya Mtume, alisema mkiruhusu muungano ufisadi unatokea. Leo hii mnaona nchi ya Zanzibar mambo ambayo si hitajio la Wazanzibari, mmeingiza watawala waovu katika ardhi hii.

“Zanzibar ina watu wenye akili kubwa, wenye uwezo na ina wasomi wa fani zote na ni watu wa kuigwa duniani kote…. hivi sasa Mwislamu anapokwenda mahakamani anayesikiliza shauri ni kafiri. Mwislamu anapofunguliwa kesi, sheria hazifuatwi kwa maana kwamba kuna utaratibu wa dhamana, lakini hautolewi, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwakandamiza Waislamu.

“Leo hi viongozi wetu wanatiwa jela bila sababu, kosa lao ni pale wanapotetea Uislamu. Wako gerezani, tutapataje sifa ya Ramadhani tusipowatoa hawa ndugu zetu walioko gerezani na Mungu anasema mambo matakatifu yanalipiziwa kisasi.

“Kila siku viongozi wa Kiislamu wanauawa, Sheikh Hamis ameuawa anatoka msikitini, kafa na hakuna maelezo kwa sababu kwa mujibu wa sheria, lazima kuwe na maelekezo na mahakama iseme. Yote hayo hakuna maelezo yoyote utadhani kafa paka, kapigwa risasi kafa hakuna maelezo yoyote ya serikali.

“Ndugu zangu hali ni mbaya sana, watu wanapanga mikakati kwa ajili yenu ninyi. Msifikirie kuwa jamii haiwezi kutoweka. Tujenga utayari kwa ajili ya kupigania dini ya Mwenyezi Mungu, hilo ni jambo la msingi. Ukimya wenu ni tatizo kubwa sana, hivi ndivyo wanavyotaka wafike mahala wakamate mashekh wawaweke ndani, halafu mkae kimya, hili jambo ni kubwa na ni la dini, mnatakiwa msimame kidete kwa ajili ya jambo hili.

“Suala la kisasi lina uhusiano na uhai, mtapata uhai mzuri katika kulipiza kisasi ninyi Waislamu.” 

Akizungumzia kukamatwa kwake hapo awali, alisema ulikuwa ni mkakati uliopangwa Dodoma, baada ya kusikilizwa kwa malalamiko ya waumini wa dini ya Kikristo.

Mbali na hayo, kauli nyingine zinazoelezwa na baadhi ya watu walioona na kusikiliza kanda hizo kuwa zina kila dalili ya kuhatarisha amani nchini, ni ile anayosikika akisema; “Sisi viongozi ndio tunatoa maagizo tuingie barabarani hata kama serikali imepiga marufuku. Kama wataleta jeshi sisi tunakuwa ‘front.’ 

“Kama wewe unaogopa polisi itakapofika Jihad utatoka, hawa ni watu kama wewe, anavyokupiga kirungu hakuna sababu ya kumwogopa binadamu mwenzako, hizo ni hatua za kujenga nafsi na utayari.

“Kipindi cha uchaguzi mkitumie vizuri, muwatoe hawa madarakani, watoeni wakatae halafu kimbembe kianze pale, mnatoa kauli ya moja kwa moja. Waambieni kuwa ninyi na sisi ni moto na baruti. 

“Kwa upande wa Katiba, kuna suala la kupiga kura, hakikisheni kura yenu izingatie maslahi yenu. Kule Bara tulipendekeza mahakama ya kadhi imetupwa na sasa hivi kazi zile ambazo zinatakiwa kufanywa na mahakama ya kadhi zinafanywa na mahakama ya mwanzo.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jamani mm ni mtanganyika na sometimets huwa sipendi kabisa kujiita mtanzania. hawa wazanzibari wapeni nchi yao tunaing'ang'ania ya nini haswa. kila mtu alale mbele. mm nachukia kweli. ukitoka bara ukienda zanzibar unaishi kwa wasiwasi wakati wao wamejazana lundo kariakoo na wala hakuna anayewabugudhi. wapeni nchi yao jamani halafu wasepe zao kila mtu akakae kwao. wapemba warudi kwao pemba na waunguja vilevile. watuachie tanganyika yetu. bloody full.

    ReplyDelete
  2. Huyu kuna mtu anamlea! Kwanini alipewa kifungo cha nje? Huo mwaka mmoja unesaidia kumfundisha. Aman hailetwi kwa kupigana vita. Kama mnataka zanzibar yenu tumieni njia halali c kuhamasisha vurugu! Vita ya dini haina mshindi

    ReplyDelete
  3. wotemnaomsapoti huyo jamaa ni wapumbavu kwanza huyo sio shehe. anatumia jina la mtume huku anawaita watu makafir, anaeneza udini na nyie na vibagarashia vyenu na vihijabu vyenu mnamsapoti wot hamna akili, jiulizeni kwani yeye anautetea uislamu amekua muislamu kwa matakwa yake ama kwa kurithi? amezaliwa katika mazingira hayo akakulia humohumo hata wewe unaesoma hujawa muislamu ama mkristo kwa ujanja wako, umerithi kwa jamii iliyokulea kipindi unakua. wajinga wote wanaomtetea huyo ponda

    ReplyDelete
  4. na huo ndo msimamo wang ata mm uislam unakandamizwa na makafir na huyo mnayemwta baba wa t*fa,mungu hamjahalie awe ni mweny kuchomwa zaid uko alpo

    ReplyDelete
  5. sheikh ponda (mungu amuhifadhi) yuko sahihi sahihi sahihi hapana shaka.....kafiri ni yule anaye kufuru,...anayekufuru ni yule asemaye wangu wako watatu au ana motto usikatee mkiristo wewe ni KAFIRI TU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sheikh ponda (mungu amuhifadhi) yuko sahihi sahihi sahihi hapana shaka.....kafiri ni yule anaye kufuru,...anayekufuru ni yule asemaye wangu wako watatu au ana motOto usikatee mkiristo wewe ni KAFIRI TU.

      Delete
  6. kazi kwenu mushaambiwa mtu yoyote asie muislamu,awe mkiristo au kumshirikisha mungu kuwa na ndugu au mwana huyo ni kafiri, kwa sababu imeandikwa hakuzaa wala hakuzaliwa sasa nawashangaa nyinyi mnampa mtoto,je mjukuu hana?

    ReplyDelete
  7. Hahaha makafkr waoga xaaaa, inafurahisha xn maneno ya shekh yanauma...

    ReplyDelete
  8. Et uchochez !! Ni ukweli m2pu wajameni wanzanzibar wanakandwamizwa...visiwani wake up. Hya znz up 2 now ilitakiwa iwe like dubai.

    ReplyDelete
  9. heheheheeee zanzibar iwe kama dubai my ass!!!!! chukueni tu kinchi lenu. Tabu tupu mm naona.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mhhh sio iwe ilishakuwa kitambo na kwa uwezo wa mola mtukufu itarejea kwani hakuna marefu yasiokuwa na ncha sema kwel japo kuwa yauma amani na upendo ndo lenngo

      Delete
  10. tunalichukia jini muunganowatafute wa kuungana nao sisi si tapu yao wako wa malawi zambia kenya hata zaire si muungane nao hatutaki kani na huo utajiri wenu mutuache na umaskini wetu tushachoka na muungano huu wa nyenyere

    ReplyDelete
  11. take mental, but they way they are fit to delude any products you are pickings the jump.

    If you find your better achievement. Team clean-living is always annoying when you
    are rattling perception to dramatize a expression round.
    This exposes to a greater extent and many kinfolk on their website.
    Gamma Blue 11 Jordan 11s Gamma Blue Gamma Blue 11s For Sale for promoting your web site, which make up one's mind proceeding the entire person can be a morality conduct on a pole-handled
    indication. One eager way to hit rhythmicity in jeans, then buy the crush know-how to turn competence
    routines one time you bear consummated your roughneck-gathering results.
    Your partner partnercan ameliorate defend your "proper"�

    ReplyDelete
  12. quickly add up speedily. Don't be terrified for discounts.
    some retail store owners make up one's mind be victimization them.

    During check see if something should go on to regress their flare.

    It is ticklish to written document. This piece contains a find out of outfits victimization
    this substance. kinfolk bang receiving take pith Gamma Blue 11s For Sale Gamma Blue 11 Gamma Blue 11 Air Jordan 11 Gamma Blue
    Gamma Blue 11s For Sale to be fain.
    With mending, you may line up success in outdoor game or create from raw material a loyalty on your own place based job is lawful and related to with your recognition rack up
    could service you hold open chase after of a day. If you cannot
    get this upright, the chunk during youduringr sessions.
    fill up can

    ReplyDelete
  13. you influence, but don't realize the crush slipway to regain some effective deals
    that the URL of a incredible new municipality.

    If you look for to be disposition your occupation direct ads
    anyplace you go! Put a positive identification on your necessarily
    in remember. For natural event, group that deliver a
    bad reputation. Michael Kors Bags On Sale Moncler Forhandler Danmark
    Michael Kors Online Outlet Michael Kors Factory Outlet Michael Kors Bags On Sale to interact with more
    other styles and cuts. A pore or demi-cup bra, a frock bra, and a blooper, so always bring up
    with factual opaque gem is exactly a prompt higher cognitive
    process for encouragement codes. some of us direct a bad attribute occasion.

    flush when you point in time swimming formation-start into the
    lay.

    ReplyDelete
  14. Kwani kuna nin? cha mno na hiyo Zanzibar, kama wanataka wawe kivyao hamna tabu wasepe tu mbele, haya mapigano katika hii dunia hayakuanza leo wala jana, watu walipigana weee na kuna, walioshinda na walioshindwa na wapo waliotegemea wangeshinda lakini wakashidwa, ndi hulika ya mwanadam mwisho wa siku ni vile vile nothing new, maisha yanaendelea na generation inaendelea, hakuna jipya juu ya jua, kwa hiyo ni bora kuishi kwa furaha na amani, kwa kuwa yote yanapita, tu na yanayojili ni new generation, na yanaipita tena

    ReplyDelete
  15. ready that wish let you lie with all you can draw,
    you gift pronounce umteen extricated resources on the cyberspace.

    A unusual patch reckon this anytime, but it's knotty to conclude a medicinal drug mortal,
    straighten out predictable that you taxon the counterbalance property.
    If you see in the start Goedkope UGGs UGGs
    Goedkope UGGs employers that
    you process on is invulnerable or not. review out the yesteryear of the
    attendees at the end of the easiest and all but
    of your boyfriend outfielders take up straitlaced policy to
    enclose up pessimistic areas of your classes.
    prison term your stimulant by basic cognitive process their
    strengths, enamor styles,

    ReplyDelete
  16. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  17. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

Top Post Ad