AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Aidha Sugu alisema ilikuwa vigumu kuvumilia konde alilopigwa na askari wakati akitolewa nje kwenye vurugu zilizotokea bungeni hivi karibuni, ndiyo maana aliamua kulipiza kisasi kwa kutaka kumpiga ngumi na si kichwa kama anavyodai askari.
‘Sugu’ alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa Chunya Mjini kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dk Willibrod Slaa ambapo viongozi hao wapo ziarani mkoani Mbeya wakifanya mikutano na wananchi kwa lengo la kuwaeleza ukweli wa kilichomtokea Sugu na wabunge wengine bungeni hivi karibuni.
‘ Sugu’ alidai kuwa Ndugai ni adui wa wapinzani bungeni na kwamba kwa vyovyote vile ilikuwa vigumu kuvumilia kwa mtu yeyote baada ya askari kuanza kupiga wabunge kutokana na amri ya Ndugai.
Naye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema kitendo alichofanyiwa Sugu hakikuwa kibaya kwake peke yake, bali hata wananchi waliomchagua.
Hata hivyo, Dk Slaa alisema kwa upande mwingine ili heshima ya Bunge lolote lile duniani iwepo, ni lazima wabunge watandikane makonde ndani ya Bunge na si vinginevyo hivyo hashangai kwa kilichotokea kwa Sugu bungeni.
Dk Slaa, alimjia juu Ndugai akisema alikiuka Kanuni za Bunge kwa kitendo hicho na kubainisha kwamba kanuni za Bunge zipo wazi kabisa kwamba iwapo itatokea vurugu ndani ya Bunge anachotakiwa kukifanya ni kuahirisha Bunge kwa wakati huo.
Pia alisema askari ambao ni wapambe wa Bunge ‘Sargent at arms’ ndio wenye mamlaka ya kuingia ukumbini na endapo itatokea nguvu ya ziada hao ndio wanaotakiwa kisheria na siyo kuwaita askari wa nje ya Bunge kuingia ndani.
Dk Slaa alisema kitendo kilichofanywa na Sugu pamoja na wabunge wengine ni cha kijasiri na aliwataka kutokurudi nyuma na misimamo yao bali waendelee kusonga mbele.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
jaribuni kuongea kiswahili fasaha kwenye R mnaweka L kwenye L mnaweka R eti fikilieni (fikirieni)kufikilia (kufikiria)
ReplyDelete