WABUNGE ZITTO KABWE NA LEMA KATIKA VITA YA MANENO BUNGENI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dodoma: Wabunge Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya maneno ambayo chanzo chake ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha wabunge (briefing) kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii.

Lema akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa kutoa maneno ambayo yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa yakimlenga Zitto kuhusu hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba ana ukwasi ambao unapaswa kuhojiwa.

Gazeti hili lilimtafuta Lema likirejea taarifa iliyotolewa na Zitto akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao hicho cha wabunge wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye.

Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akisema:

“Mimi sikumtaja mtu, kwahiyo kama kuna mtu analalamika hilo ni suala jingine, ila mimi nilimaanisha nilichokisema”.

Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa msimamo wa Lema ulikuwa unapingana na wabunge wengine wa Chadema, ambao waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.

Zitto alisema kuwa yeye mwenyewe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.

“Mimi sipokei posho kabisa, posho za vikao na ndiye mbunge pekee ambaye hapokei posho ya vikao tangu mwaka 2011,” aliongeza Zitto, ambaye anahudhuria mkutano unaozungumzia uendeshaji wa Serikali kwa uwazi huko London, Uingereza.

Zitto alisema malipo ya wabunge mpaka sasa ni makubwa sana ukilinganisha na hali ya wananchi wakati Serikali ikishindwa kulipa vizuri walimu na wauguzi.

“Hatuwezi sisi kama wabunge kuanza kulilia posho, wakati wananchi wetu hawana maji, hatuwezi kulilia posho. Mbunge anayetaka posho zaidi akafanye kazi nyingine na awaachie wanaoweza kuwakilisha watu waendelee,” alisema Zitto.

Lema, hata hivyo, alisema kwamba katika mkutano huo aliweka bayana kwamba umasikini siyo uzalendo na kusisitiza kuwa wabunge wanapaswa kuwa na maslahi bora na wakati huohuo wana wajibu wa kuwatetea watumishi wengine wa umma.

“Nilisema huwezi kuzuia taasisi moja kupewa maslahi bora eti tu kwa sababu watumishi wengine hawalipwi vizuri, ni haki wabunge kulipwa vizuri na wakati huo wapiganie maslahi ya watumishi wengine,” alisema Lema na kuongeza:

“Kwahiyo nikasisitiza kwamba nawashangaa wale ambao wanakataa posho ya Sh80,000 na ukienda kuchunguza wanakatwa fedha zote kutokana na mikopo waliyochukua, lakini bado wakija sehemu kama Arusha wanalala kwenye hoteli ya gharama kubwa kati ya Dola za Marekani 150 na 600”.

Alisema katika mazingira hayo kunakuwapo maswali mengi yasiyokuwa na majibu na kwamba mbunge wa aina hiyo alitakiwa anapokuwa katika mji wowote nchini aishi katika hoteli yenye thamani kati ya Sh20,000, 30,000 na hata Sh50,000.

“Kwa hiyo ikiwa unakataa posho ya Sh80,000 halafu unalala chumba cha Dola 600 hustahili kupata credibility (sifa) stahili, ni unafiki tu na kutafuta sifa za kipuuzi,”alisema Lema.

Alisisitiza kwamba wabunge wa Tanzania hawalipwi ipasavyo na kwamba kudai malipo ya ziada hakuwaondolei wajibu wao wa kuwatetea watumishi wengine wa umma ambao pia malipo yao ni kidogo.

“Kuna hatari ya kuona kwamba Sh80,000 au Sh200,000 ni fedha nyingi, ni kwamba kama sisi wabunge tutalipwa Sh50,000 basi maana yake ni kwamba walimu au polisi tutaridhika wakilipwa hata Sh10,000,”alisema
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tatizo la lema uwezo wake wa kufikiria ni mdogo kuliko uwezo wa kulopoka

    ReplyDelete
  2. Pumbavu sana lema wewe ni kama nani ulipwe 50,000 na walimu wanaokuweka hapo bungeni na hiyo elimu yako walipwe 10,000.kweli viongozi kama nyie mnahitajiwa kupigwa chini sawa na bibi yako ANNA MAKINDA huwezi kuwawakilisha masikini wakati wewe unapokea kila siku posho ambayo si chini ya 80,000.vijijini watu wanahitaji huduma bora kama umeme,maji na hospital wakati wewe unapiga domo na kupokea fedha kibao.nafikili wakati umefika wa viongozi wetu kuwa na hali ya kujitolea na kuwafikilia wananchi wanaoteseka.

    ReplyDelete
  3. Pumbavu sana lema wewe ni kama nani ulipwe 50,000 na walimu wanaokuweka hapo bungeni na hiyo elimu yako walipwe 10,000.kweli viongozi kama nyie mnahitajiwa kupigwa chini sawa na bibi yako ANNA MAKINDA huwezi kuwawakilisha masikini wakati wewe unapokea kila siku posho ambayo si chini ya 80,000.vijijini watu wanahitaji huduma bora kama umeme,maji na hospital wakati wewe unapiga domo na kupokea fedha kibao.nafikili wakati umefika wa viongozi wetu kuwa na hali ya kujitolea na kuwafikilia wananchi wanaoteseka.

    ReplyDelete
  4. Pumbavu sana lema wewe ni kama nani ulipwe 50,000 na walimu wanaokuweka hapo bungeni na hiyo elimu yako walipwe 10,000.kweli viongozi kama nyie mnahitajiwa kupigwa chini sawa na bibi yako ANNA MAKINDA huwezi kuwawakilisha masikini wakati wewe unapokea kila siku posho ambayo si chini ya 80,000.vijijini watu wanahitaji huduma bora kama umeme,maji na hospital wakati wewe unapiga domo na kupokea fedha kibao.nafikili wakati umefika wa viongozi wetu kuwa na hali ya kujitolea na kuwafikilia wananchi wanaoteseka.

    ReplyDelete
  5. Lema bado kabisa co,alichaguliwa na kupita kwa kuwa wananchi walishachoka na ccm,wananchi walitegemea kuwa lema angekuwa mtetezi wa wanyonge lakini kumbe porojo nyingi na kujifanya mmbabe,mwaka 2015 ajipange kwani hatuoni anachokifanya

    ReplyDelete
  6. Ilove u xna Zitto ni coz ni mtu asiyesahau alikotoka endelea hivyo hivyo my brother utafika mbali.

    ReplyDelete
  7. sidhani kwamba tuliwachagua ili mkapeane psho ambazo mnaona nilazima mlipwe tuliwachagua mkatuwakilishe ili wananchi tupate maisha mazuri lakini nyiye kila siku mnadai posho kwaa kazi gani ambyo mmetufanyia sisi ambao tumewachagua tunaomba mfanye kazi ya uwakilishi ili mmuweze kututetea katika maslahi nyiye mnapata posho zanini kwakazi gani kuliko huyo mwalimu ambaye ndiye alitakiwa apate hizo posho kwani kazi yake ni muhhimu kwa kila mwanachi hata nyie mlioko huko bungeni bila huyo mwalimu usingekuwa hapo ulipo wanafuzi hawana waalimu wakutsha hakuna madawati kwanini hizo psho msizipeleke kwenye mashule zikanunulia madawati kama kweli muwatetezi wawananchi

    ReplyDelete
  8. Yan we lema kwel ni mtanzania?? Na unajua kwel jns wananch wa kawaida wanaivyoish?? Mlo m1 kwa cku unaweza ucupate. Watu wanauana kw tsh 500 jaman tembeen muone maisha halis ya mtz jns yalivyo..yan kumbe huna tofaut na spka.. C 2lijua utakua mtetez we2 kumbe mkandamizaj..alaf unaoneka kutetea maov kw maslah ya chama na c ya mtanzania maskni..ebu imagine yule mwanach wa kawaida anaeuza pip na karanga kweny kistuli unazan anaingiza kias gan kwa cku??hata buku haifk na ndo biashara inayomfanya aish hv atakula vzr kuvaa vizr na matbabu mazur kulngana kipato chake. Eb muangalie mama anaetembeza mihogo mibich kwenye beseni then jilinganishe na wewe kutokana mshahra unaopata pamoja na posho unayoitaka!!! Bro zito fanya kaz achana nae huyo anakupotezea muda wa uwajbkaj..

    ReplyDelete
  9. Mkiambiwa Chadema chama cha wachaga mwakataa. Hivi mchaga anaweza achia hata shilingi kwa ajili ya wenye njaa au wenye shida, achilia wagonjwa. Mh wengi wanafata pesa tu huko bungeni hawana lolote, hawajui kuwa vijijini kuna watu ambao kipato chao hakifiki elf 10 kwa mwezi. Punguzeni posho zisaidie japo madawa na pia walimu waliowainua hadi hapo mlipo.

    ReplyDelete

Top Post Ad