RAGE AWEKWA KITI MOTO NA SIMBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


 KAMATI ya Utendaji Simba ‘iliyoridhia kujiuzulu’ jana usiku kwa mara nyingine ilikutana ghafla kwa ajili ya kuweka msimamo wa pamoja, kabla ya kutoa ‘tamko zito’ leo ambalo ndilo litakaloamua mustakabali wa klabu hiyo. Juzi usiku, pia kamati hiyo ilikutana kwa ajili ya kuweka mambo sawa, kwani wanaamini wao ndiyo wanaoweza kuiangamiza au kuibeba Simba kwa sasa. Kufanyika kwa kikao hicho, kumethibitishwa pia na Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang'ale ‘Mzee Kinesi’ aliyekiri, kila kitu kitajulikana leo, pale watakapoweka mambo hadharani. 

Kamati hiyo ‘iliamua kumuweka mtu kati’ Ismail Aden Rage waliyemsimamisha uenyekiti bila mwenyewe kuwepo, huku tuhuma zake moja baada ya nyingine zikichambuliwa kwa kina. Novemba 19, kamati hiyo ikiongozwa na Itang’are ilimsimamisha Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage kwa kile kilichodaiwa kwenda kinyume na katiba ya klabu hiyo ikiwemo kuahirisha mkutano wa kujadili katiba ya klabu. Hali hiyo ya kusimamishwa ilitokea huku mwenyekiti huyo akiwa hayupo nchini jambo ambalo lilionekana kama kinyume cha katiba, huku baadhi ya wanachama wakipinga kitendo hicho. Mara baada ya kurejea Rage, aliuambia umma kuwa kikao kilichomsimamisha hakina mamlaka yoyote hivyo ataendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo mpaka uchaguzi utakapofanyika. Mzee Kinese alisema, katika kikao cha jana usiku watajadili mambo mbalimbali yakiwemo mwenendo mzima wa timu yao ikiwemo kukaa kambini pamoja na kumjadili kocha wao mpya Zdravko Logarusic raia wa Croatia ambaye Rage hamtaki. “Kesho (leo), majibu yatapatikana juu ya hatma ya Simba pamoja na mgogoro uliopo baina ya mwenyekiti wetu na Kamati ya Utendaji ambayo itajadili mambo mengi ikiwemo kuiweka timu kambini,”alisema. Alisema, katiba ya Simba inasema, mwenyekiti, makamu mwenyekiti au mjumbe yoyote wa Kamati ya Utendaji kama watendaji hao hawapo na uwezo wa kuongoza kikao, ambacho kina uwezo wa kumsimamisha mjumbe yoyote kama amekwenda kinyume na matakwa ya klabu. Kutokana na kifungu hicho anasema, Rage hajaonewa na hana uwezo wa kutoitambua Kamati ya Utendaji ya Simba kutokana na ‘maamuzi’ waliyoyafanya. Alisema, anaamini mambo yote yatakwenda sawa na mgogoro utamalizika ili kuweza kuijenga timu ambayo itaweza kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara. Rage ambaye ametakiwa na TFF kuitisha mkutao mkuu wa Simba kabla ya siku 14 na kukataa, hivi sasa yupo Uingereza ambako amedai anakwenda ‘kula kuku’
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad