CCM KIGOMA WAMUUNGA MKONO ZITTO ZIDI YA CHADEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kigoma Mjini kimeunga mkono hatua ya Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA aliyevuliwa madaraka, Zitto Kabwe kusimamia demokrasia na matumizi sahihi ya fedha katika chama chake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Kwa Noti Ujiji Mjini Kigoma, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kirumbe Ng’enda alisema kuwa Zitto alikuwa sahihi katika kusimamia mambo hayo makubwa mawili.
Alisema kuwa CHADEMA kama chama ambacho kinajinasibu kusimamia demokrasia nchini kilipaswa kuonesha kwa vitendo utekelezaji wa jambo hilo, lakini badala yake baadhi ya viongozi wa chama hicho wameonesha kuwa chama hicho hakitekelezi demokrasia.
Ng’enda aliongeza kuwa kitendo cha kutangaza kuwa na nia ya kuwania uenyekiti kwa Zitto imekuwa tatizo kubwa kwa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, hali ambayo uongozi wa CHADEMA umeona ni uhaini na kuamua kumvua madaraka.
Aidha akizungumzia matumizi na usimamizi wa fedha za ruzuku ambazo vyama vya siasa vinapewa Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM alisema kuwa hilo ni suala la kisheria na ni lazima kila chama kioneshe matumizi sahihi ya fedha hizo kwa kuwa na taarifa ya mahesabu iliyokaguliwa ambapo Zitto kama Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali analo jukumu la kusimamia na kuwasilisha bungeni taarifa hizo.
“CHADEMA wanashangaza sana badala ya kuonesha taarifa iliyokaguliwa wanaanza kumsulubu Zitto kwamba anawasaliti, mara anatumiwa na CCM kuwahujumu, yote hiyo inaonesha hakuna demokrasia wala utawala bora kwa viongozi wa chama hicho,” alisema Kirumbe Ng’enda.
Awali akizungumza katika mkutano huo Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kigoma Mjini, Zuberi Mabie alisema kuwa CHADEMA imeonesha haina ukomavu wa kisiasa wala utawala wa pamoja na ndiyo maana baadhi ya viongozi kwa kuona kama chama ni mali yao hawataki kukosolewa.
Mabie alisema kuwa kukosolewa kwa viongozi ni jambo la kawaida na kwamba CHADEMA inakosea kwa kiasi kikubwa kumsulubu Zitto ambaye ameonyesha msimamo na uzalendo wake kwa Taifa badala ya chama kwa kusimamia utekelezaji wa sheria na katiba ya nchi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii sio habari, wangesema hawamuungi mkono ndio ingekuwa habari, what do u expect from magamba zaidi ya kushangilia migogoro ya cdm!

    ReplyDelete
  2. Sasa unategemea nn? Vita vya panzi neema kwa kunguru!

    ReplyDelete
  3. ukweli unabak palepale zito ana makosa gani?

    ReplyDelete
  4. Cdm ni kuma mliwavua peke yenu sa ivi ooh! ccm walikuwepo, chama mnakibolonga wenyewe na uroho wenu afu mnasingia wa2 chipi zenu shenz

    ReplyDelete
  5. magamba wenzake hao, utasikia tu keshokutwa kavua gwanda na katwika GAMBA!

    ReplyDelete

Top Post Ad