NASSARI AFICHUA MIPANGO YA KUMBAMBIKIZIA GODBLESS LEMA KESI YA MABOMU ARUSHA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari (CHADEMA), amesema Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Bw. Godbless Lema yupo katika hatari ya kubambikiwa kesi.

Alisema ipo mipango inayosukwa ili kumhusisha Bw. Lema na milipuko ya mabomu katika mikutano ya chama hicho, eneo la Soweto na ule wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, mkoani humo.

Bw. Nassari aliyasema hayo bungeni Mjini Dodoma jana katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na kuongeza kuwa ni wajibu wa Serikali kusimamia haki badala ya kuwabambikia kesi wanasiasa kwa lengo la kudhoofisha vyama vya upinzani.




Alisema kwa mara kadhaa, amewahi kutembelea magereza na kujionea vijana wengi wakiwa ndani bila hatia na kutolea mfano wa kijana ambaye alikamatwa na kuwekwa mahabusu akihusishwa na ulipuaji wa bomu Soweto na Olasiti.

"Huyu kijana yupo tayari kutoa ushahidi...alikamatwa Arusha na kupelekwa Mwanza, baadaye alihamishiwa mkoani Shinyanga ambako aliminywa sehemu zake za siri na kuvunjwa mguu ili amtaje Lema kuwa alihusika na matukio hayo," alisema.

Bw. Nassari alimtaka Bw. Pinda kutoa ufafanuzi juu ya Serikali kuwabambikizia watu kesi ili kuvidhoofisha vyama vya upinzani badala ya kusimamia upatikanaji wa haki kwa raia wake.

Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema si nia ya Serikali kutaka kuwabambikizia watu kesi ambapo mambo yaliyotokea Soweto na Olasiti si madogo na yeye hana taarifa za suala hilo.

Alisema Serikali inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watu waliohusika na milipuko hiyo na

kama kuna Mbunge anayejua kila kitu ni vyema akatoa taarifa hizo ili ziweze kupelekwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

"Kwa kweli siwezi kujibu swali hilo...Mheshimiwa Nassari anajua kila kitu na mimi sina taarifa lakini si nia ya Serikali kuwabambikizia watu kesi ni vyema uandike maelezo yako kwa maandishi ili niwape wahusika ambao ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi wachunguze," alisema.

Kwa upande wake, Bw. Lema alisema amekuwa na wasiwasi juu ya suala hilo kwani yeye hausiki na jambo hilo na mhusika yupo ambaye alilazimishwa ili amtaje yeye.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya MACCM yanafikili kuwabambikizi watukesi ndiyo suluhisho! hayajui yanaongeza wigo wawainchi kuichuki serikali, waacheni wawabambikizie kesi 2015 tuta yadhibu hayamaccm.

    ReplyDelete
  2. yamesahau kwamba Mungu yupo.

    ReplyDelete
  3. MIJITU MINGINE BWANA HATA KISWAHILI HAIJUI HARAFU INAKOMETI UTUMBO, SIASA ITAKUPELEKA WAPI WEWE NA KAA UKIJUA KUWA HAKUNA MTU MWENYE UCHUNGU NA NCHI HII KAMA UNABISHA REJEA KWENYE CHANZO CHA MIGOGORO YA HAO AMBAO UNAFIKILI NA WANAJIFANYA WANA UCHUNGU NA NCHI.
    Wanafalsafa wanasema binadamu ni muovu hivyo tambua wanasiasa wote ni wamoja hasa wa nchi zinazoendele.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We matako ya bibi yako! Hata wewe Kiswahili hujui! siyo "harafu" ni "halafu", pia kwenye Kiswahili sanifu hakuna neno linalosomeka "unafikili" ni "unafikiri" ....
      MKUNDU WAKO!!!!!

      Delete
  4. MIJITU MINGINE BWANA HATA KISWAHILI HAIJUI HARAFU INAKOMETI UTUMBO, SIASA ITAKUPELEKA WAPI WEWE NA KAA UKIJUA KUWA HAKUNA MTU MWENYE UCHUNGU NA NCHI HII KAMA UNABISHA REJEA KWENYE CHANZO CHA MIGOGORO YA HAO AMBAO UNAFIKILI NA WANAJIFANYA WANA UCHUNGU NA NCHI.
    Wanafalsafa wanasema binadamu ni muovu hivyo tambua wanasiasa wote ni wamoja hasa wa nchi zinazoendele.

    ReplyDelete
  5. nassari uko vizuri jembe nkukubal

    ReplyDelete
  6. Matako yako ndo yako vizuri,anakufira huyo

    ReplyDelete
  7. mimi sijui nyie wengine mmesoma msingi kwenye shule gani, kwanini unaweka herufi "L" kwenye neno ambalo "R" ndiyo inatakiwa itumike, hayo ndiyo matunda ya ccm kuwapatia elimu duni halafu bado mnaishabikia, wewe badala ya kuandika "halafu" unaandika "harafu"? harafu ndiyo nini? rudi shule ndugu yangu aibu!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio ccm ni we mwenyewe rafuzi yako au kabila fulani sio ccm koma kabisa au basi tuseme chadema nyau wewe

      Delete
  8. mbuzi we kama cyo ccm nani sasa? Chadema iko madarakani? akili fupi tu ndo maana mtabaki kuibiwa na kulalamika kila siku kama mabwege tu, au wewe ni mmojawapo wa mafisadi?

    ReplyDelete

Top Post Ad