OKWI "NIPANGENI MECHI YA SIMBA NA YANGA NIWAONESHE SIMBA MIMI NI NANI"

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
 Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama jana ‘ulifurika’ mashabiki wa Yanga waliokuwa na shauku ya kumwona mshambuliaji wao mpya Emmanuel Okwi akifanya mazoezi na timu hiyo.

Okwi alitua nchini juzi Alhamisi tayari kuitumikia klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani baada ya kutokea sintofahamu kuhusu uhamisho wake wa kutoka SC Villa kuja Yanga.

Si bajaji, pikipiki achilia mbali magari yaliyofurika kwenye uwanja huo huku Okwi mwenyewe akisema, “Nimefurahi sana na mapokezi niliyopewa na viongozi na mashabiki wa Yanga, nitafurahi kama nitacheza mechi ya kesho,” alisema Okwi ambaye jana alifanya mazoezi kwa mara ya kwanza na Yanga.

Akisisitiza umuhimu wa yeye kucheza alisema, “Mrisho Ngassa nimecheza naye Simba, Hamis Kiiza tunacheza naye timu ya taifa (Uganda), hakuna wasiwasi, mimi nikipangwa nao tutacheza kwa uelewano sana pale mbele  na nitafunga.”

Alisema kwa jumla anaijua Yanga vizuri na anajua uchezaji wa wachezaji wake wengi, hivyo anaweza kucheza vizuri katika mfumo wa timu hiyo.

“Unaweza kuitwa timu ya taifa, siku mbili kabla ya mechi na wakati mwingine unakuta wachezaji wengi hujawahi kucheza nao kabisa, lakini mnafanya mazoezi siku moja mnaelewana na mnacheza vizuri,” alisema Okwi.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo Ernie Brandts alisema Okwi ni mwepesi na anakasi na anajua kutengeneza nafasi za kufunga mabao na atampanga katika mchezo wa leo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao.

Jezi za Yanga zenye jina la Okwi zimetapakaa na zimekuwa zikigombewa kama njugu na mashabiki wa klabu hiyo ambayo mara zote walisikika wakiimba Okwi... Okwi...

Na kabla ya kuanza mazoezi, Brandts alimtambulisha, Okwi kwa wachezaji wenzake na benchi la ufundi.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. PIGA SIMBA HAYOOOOOO! HIYO NDO DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS BANA,CHEZEA YANGA WEWE!

    ReplyDelete
  2. labda upangwe na bb yko ndo utamfunga lkn co simba kubwa la watoto yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeona simba si ya kitoto, na hizo tano kuzirudisha mtasubiri sanaaaaaaaaaaaaaa

      Delete
  3. Vp hawajakupanga jana kumamako wewe 3 hizoooo SIMBA bab kubwa mkundu wewe!



    ReplyDelete
    Replies
    1. arudi kenya huko, alifikiri yanga ndo simba simba baba lao yanga shwain hao

      Delete
  4. Chezea simba....RAMADHAN SINDANO...NDO BABA LENU..

    ReplyDelete
  5. nyie mafala tu mnajigamba mpaka kwenye mechi za bonanza, mechi yakirafiki kupeleka timu Zanzibar kwenda kuloga kunahusu nini? msubirini EMANUEL ARNOLD OKWI mechi inayofuata ndo mtamjua ninani, c mlikuwa mnamlilia nyie mabwege, hamna hela halafu mnataka wachezaji wa gharama, maboya nyie.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad