PENZI LA DIAMOND NA PENNY LASEMEKANA BASI TENA...WEMA ATAJWA KUWA CHANZO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wamemwagana,

KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’ wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao aliliambia gazeti hili kuwa chanzo cha Diamond na Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’ kilianza kama utani.
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.

“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?” alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa Diamond. 
RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya gazeti hili kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa Diamond na Penny imebaki stori! 
 SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima Haroun ‘ Halima Kimwana’ ambayo aliiandaa Diamond.
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.
“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi,” alisikika mmoja wa waalikwa katika sherehe hiyo.
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na paparazi wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa. Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba zake.”

PENNY KIZIMBANI TENA
Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, gazeti hili lilianza na Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa ‘mzito’ kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
“Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini.”


DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji yenye maelezo yote, hakujibu.

MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu walimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye alisema hajui na hana taarifa hizo.

NDUGU WA KARIBU SANA
Baada ya mama Diamond, paparazi wetu alimpigia simu ndugu wa karibu sana na Diamond, sikiliza:
Paparazi: “Kumbe Diamond na Penny wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako mpya ni nani?”
Ndugu: “Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali, sipo Dar.

WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na wadau mbalimbali ambao walionesha kusikitika huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
“Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi tulijua hawawezi kufika mbali, maana penzi lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi,” alisema mwanamke mmoja anayejua kila kitu.

TUJIKUMBUSHE
Siku za hivi karibuni Diamond alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na mpango wa kuoa ambapo alisema kuwa hana mpango huo kwa sasa na hatarajii kumuoa yeyote kati ya wanawake wanaotajwa kwa sana midomoni mwa watu (akiwemo Penny).
Wema alipigiwa simu juzi, lakini simu yake ilikuwa ikiita ‘weee’ mpaka inakatika, inaita ‘weee’ mpaka inakatika.

Source: GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

35 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. chezea Wema ww utalala mlango wazi afu naskia Wema anamimba ya platnumz wadau tujuzane ya kweli hayo??

    ReplyDelete
  2. Sababu ya kuvunjika ni UMALAYA,USHAMBA,ULIMBUKENI NA KUTAKA SIFA leo kikowapi mtaishia kuhangaika na ujinga wenu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Au ndio.matokeo ya mganga kuelekea kufulia dogo?

      Delete
  3. tumewazoea na drama zao so hayatuhusu

    ReplyDelete
  4. NASKIA WEMA ANA MIMBA

    ReplyDelete
  5. Chezea da wema wewe lazima udeki bahari mi penda sana wewe, peny tupa kule kwenye dustben

    ReplyDelete
  6. Mapenzi ya matashtiti tupa kule. Tumewachoka na drama zao.

    ReplyDelete
  7. safi sana kama ni kweli.penny tupa kuleeee

    ReplyDelete
  8. mashabiki wa DIAMOND BURUNDI TUNAFURAHA SANA.WEMA+DIAMOND FOREVER AND FOR ALWAYS

    ReplyDelete
  9. WAWUUUU.....TUNAOMBA RUDI TENA LONDON KWENYE SPORAH SHOW.NAPENDA SANA WEMA NA DIAMOND. UJE NA WEMA PLEASE!!

    ReplyDelete
  10. UKIKUYA CONGO UKUYE NA WEMA ROHO ILITULUMAGA SANA WAKATI MULIACHANA...

    ReplyDelete
  11. WEMA WEMA WEMA C.EST BIEN JUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  12. ATA SISI WA KENYA TWAPENDA IYO COUPLE KWASABABU WANAENDANA UYO PENNY NILIZE

    ReplyDelete
  13. nikweli wema ana mimba ya diamond nimempima mwenyewe pale mwananyamaza hospt nalengo lao wanataka waoane ili penseli anywe sumu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe kichaa umenichekesha kweli. Wewe kazi yako ni kutibu mimba tu halafu unatoa siri za wagonjwa wako magazetini?

      Delete
  14. Mapenzi ya matashtiti tupa kule. Tumewachoka na drama zao.

    ReplyDelete
  15. Hahaa ukwel mtupuuuuu huko kuumwa mnakokusikia ni mimba ya shemeg dimondoooooo....ni kweli mrs dimondo mjamzitooop....pen kajizike mwenyew

    ReplyDelete
  16. Da wema uko juu hapana chezea wewe, penny hana jipya, wema na diamond forever mimi penda sana wema na diamond

    ReplyDelete
  17. Haya haya haya,sukari ya warembo Yuko single wadada changamkeni,wapi lulu kanumba na Kati ya tandale uzuri

    ReplyDelete
  18. jamani nimecheka mbavu zangu weeee!atu wa humu ndani wamepinda kwelikweli, oooh! timu wema kweli nimeamini waswahili wanasema lilia bahati siyo sura kama sijakosea hiyo sentensi sasa wema ana bahati sana ana sura nzuri na umbo zuri na zaidi ya yooote ana damu ya kupendwa na kila mtu yaani mimi sijui huyo mtoto amezaliwa vipi mimi hapa sijawahi kumwona live wema zaidi hapa ktk blog na kusoma habari zake tu,lakini nampenda balaa mimi ni mama mtu mzima tu huwezi amini ninavyopenda hii couple ya wema na diamond utadhani wanangu nadhani iko siku watakuwa pamoja maana kama wameandikiwa wawe wanandoa hata mtu afanye vipi hataweza kuzuia binadamu huwa anachelewesha tu lakini bahati iko palepale iko siku haina jina wema na diamond wataowana tu maana hii midomo ya watu wengi kuwatakia wawe pamoja lazima itakuwa one day,bealive me, one day yes wema and diamond nawapenda sana nawatakia maisha marefu yenye baraka tele na uzao mingi wa baraka mjaliwe watoto wakiume na wakike wawe na afya njema sana god bless you

    ReplyDelete
  19. maadili yameshuka sana cku hz vijana wamekuwa baiskeli za kijiji waziwazi wakiona ndio sifa. wazazi wanachangia kujifanya bize na life huku mtoto anapotea wenyewe biiiize bar wakizinduka inakuwa too late.

    ReplyDelete
  20. mama zenu nyote

    ReplyDelete
  21. PIG UP MY LOVE SISTER!

    ReplyDelete
  22. Penda sana hii couple naona kama ni ndoto vile siamini ila nakuomba Diomond siku ukija Canada njooo na Wema sijawahi kumuona Wema ila ninavyopenda couple ya Diomond+Wema utadhani nina undugu nao tunawaombea Mungu awasaidie mje muitwe mke na mme one day. Penseli kwishneiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  23. Penseli tupa kuleeee,Ana ishu huyo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ubaya Wa penseli ni gold digger,yeye penzi lake ni pesa na majumba,Hana penzi la kweli,naseeb filisika uone Kama utaona penseli au peni.

      Delete
  24. wema and diamon forever i wish one day muwe mjenge familia yenu itapendeza sana

    ReplyDelete
  25. Mamton ndo wanaweza oana mastaa, ila kibongobongo ni nadra sana. Na yaweza kuwa huyo diamond anatafuta mwanya wa kuweza kuwakwepa wote, japo mnadai anataka kumrudia wema, kwan hawez kumwaga hata kama wema ana mimba ake?!... Hyo inawezekana na kwa diamond ni k2 rahs mno, embu despite z fact warembo alopitia mastaa? Bila shaka jibu unalo kuwa jamaa hawez oa, ci peny ama wema. Mi kibongobongo nampenda BARNABA HUYU KIJANA ANA MADIR NA ANAJUA ANACHOKIFANYA, kuanzia mzik wake na ndoa ake...na wengne kama huyo, na si diamond.

    ReplyDelete
    Replies
    1. utajibeba wema na diomond forever

      Delete
  26. Diamond kama unasomaga hizi comment humu, ufanyie kazi haya mambo. Mashabiki wako wanapenda uwe na wema, na si kuruka ruka mara leo huyu, kesho yule siyo sifa kuwa Malaya mtoto wa kiume. na wewe mama diamond, utulie sasa siyo kujifanya kimbelmbele kuingilia uhusiano wa mwanao, kujishaua kwenye media oooh mi nampenda Fulani, we ndiye unalala naye? kama mapenzi ni rahisi hivyo mbona wewe huna mume?

    ReplyDelete
  27. God humu comnt ni wema tu maskini huyu penny kawakosea nn hana haki yakuogelea nae kama wenziwe?diamond bahari na ndio wanawake waogelea...

    ReplyDelete

Top Post Ad