ACHENI KUVAMIA FANI NA KUFANYA MAMBO YA AJABU KUTUHARIBIA FANI-KING MAJUTO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa mujibu wa tovuti ya mwananchi, mwigizaji nguli Amri Athumani (King Majuto),amewajia juu wanaovamia fani ya vichekesho kwa kufanya vitendo alivyosema vinatia kinyaa kuviangalia.

Alisema kwamba baadhi wa wachekeshaji wanamchukiza kwa kufanya mambo ya aibu na kujidhalilisha wenyewe, badala ya kuchekesha akiwataka wajipange kabla kuvamia fani hiyo.

“Wapo vijana wanafanya kitu ukiangalia unafurahi na kwa sisi wachekeshaji wa siku nyingi unajifunza kitu, lakini hawa wavamizi ukiangalia unaweza kutapika. Sipendi na wananiudhi. Kama vipi wajipange upya,”alisema Majuto bila kuwataja akieleza kuwa anaowakusudia wanajijua.

Aliongeza kuwa kila kazi inahitaji umakini ili iweze kuvutia na kupata soko, akilalamika kwamba wachekeshaji wanaofanya kazi hiyo ili mradi wapate fedha ya siku wanawaharibia wenzao wanaotegemea kazi hiyo kwa maisha yao yote.

Alibainisha kuwa binafsi amefanya kazi ya uchekeshaji kwa zaidi ya miaka 55 na ndiyo inayompa heshima maishani mwake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad