GIZA NENE LATANDA NDANI YA CHAMA CHA CHADEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Giza nene limeendelea kutanda ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya juzi kulazimika kuongeza muda wa kikao cha Kamati Kuu kusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake Zitto Kabwe.

Kikao hicho kiliendelea jana kikimhoji aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa Zitto Kabwe ameendelea na msimamo wake akituhumu chama hicho kuongozwa kwa ubabe.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kinachofanyika Hoteli ya Mbezi Garden jijini Dar es Salaam zinaeleza kuwa mkutano huo ulianza saa 4:00 asubuhi kwa kujadili ajenda zilizoshindwa kujadiliwa juzi, ambapo Dk Kitila alianza kuhojiwa saa 7:00 mchana.

Hata hivyo, taarifa hizo zinaeleza kuwa baada ya Dk Kitila kuingia kuhojiwa, aliwaomba  wajumbe amwite mwanasheria wake, ambaye anazifahamu vyema taratibu na sheria za chama ili amsaidie kujibu hoja.

Kazi hiyo ya Dk Kitila kutafuta mwanasheria ilichukua muda mrefu na akapatikana saa 11;00 jioni ndipo kikao kilipoanza.

Hata hivyo, kabla ya kuingia katika ukumbi huo wa mkutano, Dk Kitila aliliambia gazeti hili kuwa atatoa ufafanuzi wa msimamo wake baada ya kutoka ndani ya kikao hicho.

Hata hivyo, hadi saa 1:00 jioni jana alikuwa bado ndani ya chumba cha mkutano akihojiwa, huku taarifa zaidi zikieleza kuwa wajumbe wengi walikuwa wakimsihi Dk Kitila aombe radhi ili asamehewe, yaishe.

Baada ya kumaliza kuhojiwa saa 1:40 usiku, Dk Kitila alimwambia mwandishi  amemaliza kazi yake na anauachia uongozi kutoa uamuzi wake.

Mnyika

Awali akitoa taarifa ya kikao hicho, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika alisema kuwa Kamati Kuu ilishindwa kuwahoji Dk Kitila na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba baada ya kuondoka mapema eneo la mkutano bila ya kuaga na kuzima simu zao. Alisema kwa sababu Chadema ni chama kinachoamini katika demokrasia, waliamua kuwatafuta kwa namna nyingine na kufanikiwa kuwapata jana asubuhi.

Mnyika alisema kuwa kama mmoja wa watu hao hatafika kuhojiwa mbele ya Kamati Kuu, basi chama kitachukua uamuzi kitakachoona unafaa dhidi yake.

Mjumbe wa Kamati Kuu apigwa

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Shaaban Mwamba, juzi usiku alipata kipigo kutoka kwa maofisa wa  kikundi cha ulinzi cha chama hicho waliokuwa katika eneo ambalo mkutano wa Kamati Kuu ulifanyika, baada ya kutuhumiwa alikuwa akiwasiliana na wafuasi wa Zitto.

Taarifa kutoka kwa mjumbe mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, ilisema kuwa mtu huyo alikuwa akichunguzwa na maofisa wa ulinzi wa chama hicho muda mrefu, kutokana na nyendo alizokuwa akizionyesha zilizotia shaka.

Mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwa katika eneo hilo, alishuhudia kiongozi huyo akibebwa juu juu na maofisa hao, huku akiulizwa aliyekuwa akiwasiliana naye ni nani, kabla ya vijana wengine wa chama kumkamata na kumweka chini ya ulinzi, wakimtaka atoe ufafanuzi wa alichokuwa anakifanya.

Baada ya mahojiano ya muda mfupi, kiongozi huyo alionekana akiinuka na kwenda  kunawa kwenye bomba la maji, huku akitokwa damu mdomoni.

Taarifa zilizopatikana baadaye zilidai kuwa kiongozi huyo alikuwa akiwasiliana na mama yake Zitto na Katibu wa Zitto, Dk Alex na kwamba pia simu yake ilikutwa na ujumbe mfupi aliokuwa amewaandikia watu hao.

Gazeti hili lilijaribu kumtafuta kiongozi huyo ili kueleza sababu ya kupigwa kwake, lakini hakupatikana eneo la mkutano kwa madai kuwa alikwenda hospitali kupata huduma ya kwanza, lakini hakurudi.

Wakati suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na uongozi wa chama chake likiendelea kuwasumbua vichwa wapenzi wa chama hicho, inadaiwa kuwa baadhi wa wabunge, viongozi na wazee wa Chadema, wanataka suala hilo liishe mapema.

Habari ambazo gazeti hili lilizipata jana, zilisema kuwa baadhi ya viongozi hao walitaka Zitto aende Halmashauri Kuu ya Chadema na kuomba msamaha ili mambo yaishe.

“Walimfuata Kitila (Dk Kitila Mkumbo) wakamwambia amshawishi Zitto ili mambo yaishe nje ya mahakama, wanataka aende kwenye Halmashauri Kuu kuomba radhi. Kitila akawaambia kuomba radhi kwa kosa gani?” kiilisema chanzo hicho.

Zitto azungumza

Hata hivyo, Zitto aliliambia gazeti hili jana kuwa kumekuwa na jitihada  mbalimbali za wazee kutaka kukiepusha chama hicho na migogoro na kuwa amekuwa tayari kwa suala hilo. “Wazee walikuwa na wajibu wa kuhakikisha hatufiki hapa tulipofika. Sijui kama fursa hiyo bado ipo,” alisema Zitto.

Kuhusu uamuzi wake wa kwenda mahakamani alisema: “Nimekwenda mahakamani kutaka haki itendeke. Chama cha kidemokrasia kinanyima vipi mwanachama fursa ya kukata rufaa?

“Nisingekwenda mahakamani kama ningeona haki ikitendeka. Tatizo kubwa la chama chetu sasa kinaongozwa na mawazo ya kihuni na yeyote mwenye mawazo ya kujenga anaonekana msaliti.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. zito tumekuelewa endlea na kaz jemedar

    ReplyDelete
  2. Wapenda madaraka CDM mnaandaika na ubaguzi wenu mnaendesha kimkwe mkwe shemeji shemeji ukanda ukanda na udini udini.
    mnatoa watu sadaka
    Mtaandamwa na kila mlomtoa sadaka

    ReplyDelete
  3. Chama gani hata ukiwasiliana na mtu unapigwa mko wp wale viherehere wa hhaki za binadamu au mnamuog opa mboe maana ni kundi lake

    ReplyDelete
  4. Kweli chadema mmekoma kidemokrasia hata mtu ukipiga cm mkutanoni unapigwa kweli jeshi lenu llinanyanya raia kuliko polisi mnaowasema wabaya kila kukicha kumbe mkuki kwa nguruwe

    ReplyDelete
  5. Yaaan Chama cha Domo ma Majungu CDM hamjapata madaraka mnapiga mkutanoni.
    Mkipata madaraka si itakuwa Hatari Ua yule piga
    Mmeshavunja rekodi ya M (Paka) mpaka sasa kwa kusababisha vifa hasa vya panya

    ReplyDelete
  6. Chadema kaeni chini myamalize mnashusha hadhi ya chama

    ReplyDelete
  7. Yani zitto ukiomba msamaha ni najitoa chama chenyewe, komaa kaka haki ipo, wameshaanza kujinyea hao! Nakukubali sana........................

    ReplyDelete
  8. Uongozi wa chama hayo yapo ktk maendeleo yoyote,but also zito unapanic sana kua makini unaweza kupotea kisiasa na malengo yako kufifia

    ReplyDelete
  9. Bora hiki chama kife tu...fujo tupu mjini kumalamamake

    ReplyDelete
  10. kuma la mamake nani sasa? yaan mtu unakurupuka tu na mitusi! si ndo hilo limekuleta duniani? fala we.

    ReplyDelete
  11. Nawewe mpumbavu huna adabu mbona unatukana bora nawe ungekaa kimya mkubwa mashavu natusi ulilo tukana tukana na la baba yako uone laha wajinga wote kasoro kipenzi cha watu zitto koomaa nao usiwaogope wachawi wakubwa muacheni zitto mika 1ooo.

    ReplyDelete
  12. Nailaumu sana serikali yetu.inakuwaje watu wanapigwa kwa kisingizio cha siasa?Serikali timiza wajibu wako wa kulinda raia wote na mali zao.Kama kuna chama kinajifanya FFU kidhibitiwe mara moja kwa mujibu wa sheria.Chadema si chama cha siasa tena bali genge la waviziaji wa raslimali za Tanzania.ni mafisi yanayogombania kupata fursa ya kuposa rasilmali zetu.Hayana akili kuona kwa mwenendo huo watanzania wameyang'mua.CCM jipangeni vizuri njia ya Ikulu ni nyeupe

    ReplyDelete

Top Post Ad