UAMUZI WA YANGU KUJITOA KOMBE LA MAPINDUZI HAUKUWA WA BUSARA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imechukua hatua ya kushangaza ya kujitoa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Zanzibar katika dakika za mwisho.

Uongozi wa Yanga ulichukua hatua hiyo siku moja kabla ya mashindano hayo yanayoshirikisha timu 12 kutoka Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania kuanza.

Kwa kweli hatua hii ilikuwa ya ghafla mno na tunaamini imewakwaza na kuwapa mtihani  mkubwa waandaaji wa mashindano hayo.

Itiliwe maanani kwamba mashindano hayo ya mwaka huu ni makubwa zaidi na yamepewa uzito mkubwa kwa vile yanafanyika wakati Zanzibar inasherehekea miaka 50 ya Mapinduzi. Kitendo cha Yanga kujiondoa kwenye mashindano hayo tena dakika za mwiso kimeshangaza hasa kwa kuzingatia uhusiano wa klabu ya Yanga na Mapinduzi ya Zanzibar.

Historia inaonyesha kuwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani  Karume aliwahi kutumia fedha za wananchi wa Zanzibar katika kusaidia kujenga makao makuu ya klabu ya Yanga yaliyopo Jangwani, Dar es Salaam.

Sasa inashangaza kwa uongozi wa Yanga kusahau  historia hiyo na kujitoa katika mashindano yanayotukuza Mapinduzi hayo ya mwaka 1964.

Ukiacha suala hilo la kihistoria, mashindano hayo ya Zanzibar yalikuwa muhimu mno kwa Yanga katika maandalizi yake ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo wanashiriki mwaka huu.

Yanga ingeshiriki  mashindano hayo timu yake ingepata nafasi ya kujua upungufu na udhaifu wake kwani katika hatua za awali ingepambana na Azam ya Dar es Salaam na Tusker ya Kenya ambazo ni timu kubwa na ngumu.

Kuondoa benchi la ufundi na kuitumia kama ndiyo sababu ya kujitoa kwenye mashindano hayo hakutoshi kwani klabu kadhaa zimekuwa zikifukuza makocha lakini zinaendelea na mechi zinazowakabili.

Kama uongozi wa Yanga ungekuwa umejipanga vizuri ungekuwa tayari na kocha mpya ambaye angeitumia michuano ya Kombe la Mapinduzi kuona na kufahamu aina ya wachezaji alionao. Yanga ni lazima ijifahamu kuwa ni klabu kubwa na yenye mashabiki wengi nchini kwa hiyo inatakiwa kutafakari kwa makini kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule.

Ni dhahiri kwamba kujitoa kwa Yanga kwenye mashindano hayo kutawaathiri sana waandaaji hasa kwenye mapato kwani mechi za Yanga zilitarajiwa kuwavutia mashabiki wengi.

Lakini, kama Yanga ingejitoa mapema katika mashindano hayo na kuukataa mwaliko wa kushiriki kungewapa nafasi waandaaji kualika timu kubwa kwenye mashindano hayo na ambayo ingepata nafasi ya kujiandaa kabla ya kwenda kwenye mashindano.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inajipanga kwanza

    ReplyDelete
    Replies
    1. WOGA UMEWAZIDI,
      au milango ilifungwa mambo
      ya Issa Makongolo HAKUNA?

      Delete
  2. hayo ndo matatizo ya club zetu za tazania hawakubali walikotoka ndiomana timu zetu tunategemea wachezaji wageni kwa matatizo hy hayo hatusani vyakwetu tuache ujinga hata club za ulaya haziwasahau mashujaa wao ndio njia ya mafanikio club zetu zinapoteza kumbukumbu ndio maana soca letu zero

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usichanganye mambo
      Tabia ya kuogopaogopa anayo yanga tu,
      Simba si mchezo haogopi
      timu yoyote kama alivyo
      MNYAMA tishio MSITUNI
      sauti tu unajikojolea
      yanga eti walijua watakutana na SIMBA.

      Delete
    2. Wewe si mwanamichezo
      Tunachoongelea ni yanga,
      Wala si timu taifa.
      Timu binafsi inauwezo wa kuchukua mchezaji yoyote duniani, iwe yanga,simba, azam,
      ashanti n.k
      Na wachezaji wetu wazawa wana
      Uwezo wa kucheza matifa mengine.

      Delete
  3. cyo lazima Yanga ishiriki mashindano yote, kwani timu nyingine hazitaki kushiriki, walichofanya ni sahihi kuwapatia fursa na wengine washirika, kama Ashanti vile.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe mwoga wa kufungwa
      au katika wale waliozimia
      kipigo cha goli 3?
      Yanga,Simba kazi yao ni kucheza mpira football
      M'mekimbiaa M'meogopaaaa

      Delete
  4. na jana tumewapa milioni kumi, ambazo ni nyingi kuliko thamani ya kombe lenyewe, sasa huo siyo uungwana?

    ReplyDelete
  5. Yanga
    Imekimbia kipigo
    Bado wanawaza kipigo cha goli 3ile ni bonanza tu jamani
    Nasikia tetesi mnawashawishi waliowafunga siku ile muwachukue! Mnatafuta goli 7 mtazipata lini mvunje record? MNATIA AIBU KUTOSHIRIKI
    KOMBE LA MAPINDUZI kumbe si wazalendo!

    ReplyDelete

Top Post Ad