KWA HILI DIAMOND UNASTAHILI PONGEZI!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KWAKO,
Nasibu Abdul ‘Diamond’. Pole na kazi na mihangaiko ya hapa na pale. Najua uko bize sana na shoo za kila kukicha. Siyo mbaya, ndiyo maisha, maana bila kazi inakuwa siyo maisha tena.

Muda mrefu sana hatuwasiliani... nasikia siku hizi unapokea simu kwa nadra sana! Hata hivyo, siyo lengo langu kuzungumzia hayo. Ni kitambo kidogo hatujakutana kwenye barua.

Naamini leo ni sahihi zaidi kukufikishia ujumbe huu. Hata kama kuna mengine niliyotaka kuzungumza nawe, lakini kuna jambo ulilofanya, limenifanya niweke mengine yote pembeni kwanza.
Diamond, siri ya mafanikio ya binadamu yapo katika utoaji. Hapo kuna mara mbili; kutoa kwa wahitaji ambao hawajiwezi au kutoa kama shukrani kwa wanaochangia mafanikio yako!

Mwaka jana katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar ulifanya Tamasha la Krismasi na Ngololo ambapo pia uliwashindanisha watoto kucheza wimbo wako wa Number One ambao ndani yake kuna kionjo cha Ngololo.

Ahadi yako kwa washindi ilikuwa ni kuwasomesha watoto hao katika shule bora kama zawadi kwao. Ilikuwa ahadi nzuri sana kwako, maana wote walikuwa wakisoma katika shule za kawaida a.k.a St. Kayumba.

Ile ilibaki kuwa ahadi tu... wengi waliamini yalikuwa maneno ya kujipaisha. Kitendo chako cha kutimiza ahadi hiyo Januari 21, mwaka huu kwa kuwapeleka hao watoto katika Shule ya Kimataifa ya Afrika Mashariki (East Africa International School), iliyopo Mikocheni, Dar kimekuongezea heshima kubwa kwenye jamii.

Hii imeonesha ni kwa namna gani umetambua na kuthamini elimu. Ni vigumu sana kwa msanii mwingine kufunika rekodi hii, hata kama mwingine akija kufanya, atakuwa ameiga kutoka kwako.
Nasikia wanafunzi hao, mmoja ameingia darasa la nne  na mwingine la tano na wote kwa pamoja umeahidi kuwasomesha mpaka watakapomaliza darasa la saba.

Hongera sana bwana mdogo. Hapo umeonyesha ukomavu wa fikra wa hali ya juu. Jambo hili liwe fundisho kwa wasanii wenzako. Kumbe mnaweza kufanya mambo makubwa kwa jamii na mkajenga heshima.

Bila shaka yoyote, utakuwa umejiongezea mashabiki luluki kwa tendo hilo ambalo pengine kuna msanii hakuwahi kulifikiria. Hapo tegemea mafanikio katika kazi yako, maana umerudisha sehemu ya pato lako kwa mashabiki wako.

Hongera sana. Nadhani nikuache ufanye kazi, lakini sasa Diamond, mbona hupokei simu za waandishi kamanda? Nasikia wifi yetu  amekubana... ni kweli? Hayo tutaongea siku nyingine ila kwa hili la kuwalipia madogo ada, chukua tano!
Yuleyule, 
Mkweli daima, 

Joseph Shaluwa

GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mambo ya kawaida tu hayo usitake kumpa sifa domo bure!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama baba yako ameshindwa kukulipia ada ukaishia darasa la tano shule ya msingi nguvumali.. matokeo yake leo umekuwa dalali wa vyumba, utawezaje kuona kuwa jambo alofanya Diamond linahitaji kupongezwa..

      Delete
    2. Wazee wa chuki hamkosekani. Hujawahi hata kumpa nauli ya shule mdogo wako sababu huna kazi uko kitaa kupiga umbeya, Leo unajifanya kutoona umuhimu wa msaada alotoa Domo.

      Delete
    3. Hela za chief kiumbe hizo c amesema anamsapot kwa kila ki2 mapenzi wake diamond

      Delete
    4. Na wewe nenda kwa chief basi uombe hela uweze kulipia watu hizo Ni juhudi zake diamond acha chuki maku wewe

      Delete
  2. EARN $50 - $100 USD Daily Easy

    http://earnstart.com/?id=145518

    ReplyDelete
  3. Me mwenyewe.nampa 200 Nasibu ssna sana kama anavyo mpenda mam wake big up Mwanangu god akujalie.

    ReplyDelete
  4. kwa hilo nakupe mia tena miaaaaa hongera nasibu wa wema

    ReplyDelete
  5. Mademu wa kitaa
    www.babylanta.blogspot com

    ReplyDelete
  6. Diamond wa Sepetunga forverrrrrr

    ReplyDelete
  7. hi ndio kawaida ya wabongo mchango wa arusi kwanza elmu baadae DIAMOND upo juu brather heshima kwako ndugu

    ReplyDelete
  8. Jamani nina shida nataka nikutane na Diamond anipe angalau pesa kiasi na mimi nijisikie faraja kwa mwanangu Diamond naombeni sana natumaini huu ujumbe utamfikia na simaramoja kuna siku nilikutana nae mlimani city nikaona aibu watu walikuwa wengi nikashindwa, naomba sana mwanangu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani huyo mwnao hana baba wacha kupapatikia watu waliokuwa hawakuhusu wee!

      Delete
  9. Kwa hili hongera sana,ajitokeze mwengine

    ReplyDelete
  10. hizo shule zinazojiita international school kweli zina viwango? au ndio jina tu?

    ReplyDelete
  11. Domo kubwa kajitaidi ila apunguze msasa usoni.

    ReplyDelete
  12. Jamani mwanaume kujichubua inahusu umekua kama shoga Mxiiuuuuuuuuu na sura kama kibamia

    ReplyDelete
  13. http://internetduty.com/user/dashboard.php

    ReplyDelete

Top Post Ad