NAPE ATOFAUTIANA NA JAJI WARIOBA BUNGE LA KATIBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba, litatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo ya mtu yeyote.

Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.

Warioba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea katika Katiba Mpya.

Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba likipewa jukumu la kuandika Katiba linaweza kubadili mambo mengi, lakini kama Katiba itakuwa imeandaliwa na chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa kutobadili hoja za msingi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema: “Mchakato wote wa Katiba Mpya unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo inawezekana kabisa kuboreshwa na hata kubadilishwa kwa hoja.”

Nape alisema kulingana na sheria hiyo, Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho kadri itakavyoonekana kuwa inafaa.

“Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge hilo kwisha wananchi watapiga kura ya maoni,” alisema.

Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si kubadili hoja za msingi, Nape alisema: “Maboresho maana yake ni kubadili. Ukiwa na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?”

Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe katika uamuzi wake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hayaa kaz kwenu wenye nchi walala hoi hatatukisema kaz buretu

    ReplyDelete
  2. Nape msenge opportunist kwan ye nani nchi hii nakwambia omba mungu system ya utawala isibadilike ikibadilika utakuwa maskin wa kutupwa mbwa ww nape nape nini nape mavi

    ReplyDelete
  3. Nape yupo sahihi kabisa. Waachwe wawakilishi wafanye yao na sisi wenye nchi tutamalizia kwenye kura za maoni.

    ReplyDelete
  4. Nape is useless non sense stupid opportunist na his time is countable.yeye asubiri tu mzee wa magogoni aachie ngazi uone atakavyopigwa ngwara ya hatari.Nape ni mchumia tumbo tu huyo.

    ReplyDelete
  5. Nape mpumbavu tu. Anajifanya anajua kila kitu

    ReplyDelete

Top Post Ad