MASKINI:MBWA WA UBALOZI WAMLA MTOTO!

NI vigumu kuamini kilichotokea lakini ndivyo ilivyokuwa! Mtoto Christian Alex (6) ameuawa kikatili kwa kuliwa na mbwa wanaodaiwa kuwa ni wa Ubalozi wa Qatar nchini  Tanzania unaoongozwa na Balozi Jassim Mohammed Mubarak Daruwesh.

Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Machi 26, mwaka huu Jangwani Beach, Kunduchi jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo alishambuliwa na mbwa wa kigogo huyo alipokuwa na baba yake jirani na nyumba hiyo ya kupanga yenye nyumba nyingine mbalimbali (apartment).
MAELEZO KWA UFUPI
Inaelezwa kuwa, baba wa marehemu pia anaishi kwenye moja ya nyumba hizo akifanya kazi ya kutunza mazingira endapo mpangaji mmoja anahama. Wote wanaoishi humo wanatumia mageti mawili tu, kuingia na kutoka.
Mama wa mtoto Christian Alex akiwa amezimia wakati mwili wa mwanae unazikwa
BABA WA MAREHEMU ASIMULIA
Akizungumza na gazeti hili kwa majonzi  kwenye msiba uliogubikwa na vilio na simanzi, baba wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Alex, alisema siku ya tukio yeye alikuwa akitoka nje ya nyumba anayoishi katika ‘apartment’ hizo, lakini  ghafla nyuma yake alisikia kelele za mwanaye.
“Kwa kawaida ili utoke lazima uwe makini, kwanza ujue mbwa wako wapi? Nilipotoka nikiwa nawaangalia walipo, mara nikasikia kelele mtoto wangu analia, nilirudi haraka, nikamkuta mwanangu anashambuliwa na mbwa watatu huku tayari akiwa na majeraha makubwa.
Mazishi ya Mtoto Christian Alex (6).
“Ilibidi nimng’ang’anie mtoto ili kumwokoa ambapo pia niliokota jiwe kutaka kuwapiga, wakataka kuondoka lakini wakarudi tena na kumvamia.
“Hapo ndipo ilikuwa shughuli kwani walimfumua utumbo, wakazinyofoa sehemu zake za siri na kuziingiza midomoni huku kisogoni wakimtia kucha kali mpaka kumtoa ngozi.
“Wakati kitendo hicho kinaendelea huku nikishuhudia kwa macho, yule balozi akawa anaingia ndani, akawaamuru mbwa wake waache, walitii amri hiyo lakini hali ya mtoto wangu ilikuwa mbaya sana, akawa hasemi wala hapigi kelele tena za kuomba msaada,” alisema baba huyo huku akimwaga machozi. Inauma sana!
Mtoto Christian Alex  baada ya kujeruhiwa na mbwa wa ubalozi wa Qatar.
Akaongeza: “Mpaka sasa siamini kilichotokea, nashindwa hata niongee nini, ninachoweza kusema ni kwamba mwanangu Christian nilikuwa nampenda sana kama vile ninavyompenda mwanangu mwingine, Sabina.
“Nahisi ukiwa baada ya kupoteza mtoto wa kiume niliyekuwa namtegemea. Itanichukua muda mrefu sana kusahau kile nilichokiona kwa macho yangu. Nimeshuhudia mwanangu akishambuliwa na wala sikusimuliwa na mtu.”
Mazishi yakiendelea.
KUMBE TAHADHARI ILITOLEWA
Baba anaendelea kusimuliza: “Kinachoniuma zaidi ni kwamba, nilishatoa angalizo tangu mwanzoni wakati huyu bwana anahamia kwenye nyumba hii. Nilimwambia mwenye nyumba  amwambie huyu awajengee banda  mbwa wake lakini wakapuuzia.”
ADAKTARI WALIVYOSEMA
Baadhi ya majirani walifika eneo la tukio na kukuta sakata hilo limefikia hatua ya mbwa kutii amri ya bosi wao na kurudi kwenye maskani yao.
Walimchukua mtoto huyo na kumkimbiza kwenye Hospitali ya IMTU iliyopo Mbezi, Dar  ambapo madaktari walisema alishafariki dunia kitambo.
VILIO VYATAWALA 
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, haraka mwandishi wetu alifika eneo la tukio muda mfupi baada ya mtoto huyo kupelekwa hospitali na kushuhudia vilio vikitawala kwa kila jirani aliyepata taarifa za kifo hicho cha kusikitisha.
MAJIRANI WASIMULIA
Wakionesha jinsi walivyoumizwa na tukio hilo, baadhi ya majirani walisimulia jinsi mbwa hao wanavyowatishia amani katika nyumba hiyo ambapo tangu kigogo huyo ahamie ndani ya nyumba hiyo wamekuwa watu wa kujifungia siku nzima wakihofia mbwa hao wakali.
“Jamani huyu mtoto kafa kifo kibaya sana, mbaya zaidi mbwa hawa wamekuwa tishio kiasi cha watu kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.
“Mbwa huwa hawafungiwi kwenye banda, labda ingekuwa hivyo wasingefanya hivi,” alisema jirani mmoja huku akilia bila kikomo.
POLISI WALIVYOFANYA
Paparazi wetu alipojaribu kuingia ndani na kwenda kuongea na balozi huyo, askari waliodaiwa ni wa Kituo cha Polisi Kawe jijini Dar walitia ngumu huku ikidaiwa kuwa maelezo waliyoyaandika ni mmiliki wa mbwa kuwa mzembe kwa kuwaachia mbwa kudhuru binadamu.
MAMA MZAZI AZIMIA
Maria Mvile, mama mzazi wa marehemu Christian kwa sasa yupo katika hali mbaya tangu mkasa wa kushambuliwa mwanaye na mbwa hao utokee ambapo amekuwa akizimia mara kwa mara.
Mwandishi wetu alimshuhudia mama huyo akishindwa kuweka shada la maua katika kaburi la mwanaye kwa kuanguka na kuzimia.
MAZIKO
Safari ya mwisho ya mtoto Christian ilifanyika kwenye Makaburi ya Mburahati, Dar es Salaam ikitanguliwa na misa iliyosomwa na Katekista wa Kanisa Katoliki Mburahati, Owen Hokororo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukiri kuwa ni nyumbani kwa balozi wa Qatar nchini.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
GPL

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Rip baby boy.

    ReplyDelete
  2. Kumbe mbwa siyo filthy kama dini ya hao watu wa Qatar wanavyotuminisha. Nashangaa mtu ambaye ni mfuasi wa mtume kufuga mbwa anayekula binadamu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We unafirwa, hanithi mkubwa, una mkundu kama kisima cha kijijini, mbwa anahusiana vp na dini?? Swala la mbwa ni la mtu binafsi, nyoko we!!!

      Delete
  3. Ee mungu mwenyezi watie nguvu wazazi wa huyu mtoto, , this is so sad I can't imajin wat these people are going thru

    ReplyDelete
  4. Maskini we nae hanithi mtu sio dini,usiingize udini hapa ni MTU mwenyewe sio mstaarabu,dini imeingiaje hapo tumia akili kufikiri sio homon.

    ReplyDelete
  5. Huyo mshua mwenye hao mbwa itakua ana roho mbaya sana, yaan anashindwaje kutunza hao mbwa vizur ndan ya get, na kawaacha hadi majirani kufikia hatua ya kutokuwa huru na mzingira ya nyumban kwao, inatia hasira sana, naomba serikal ichukue hatua kali dhidi yake, isifumbie macho hata kama baloz, huo ubaloz wake isiwe kigezo. Home boy R.I. P

    ReplyDelete
  6. Ingekuwa huku marekani. Angenyea kambi, jela regardles of who you are.
    R.I.P Christian

    ReplyDelete
  7. Rip baby boy Alex inaskitisha saana

    ReplyDelete
  8. Rest in peace baby

    ReplyDelete
  9. Huyo balozi anaroho mbaya sana! Au yeye hajazaa? Tunaiomba sheria ichukue mkondo wake bila kujali hilo likatili kama lina wadhifa gani.

    ReplyDelete
  10. Huyo balozi anaroho mbaya sana! Au yeye hajazaa? Tunaiomba sheria ichukue mkondo wake bila kujali hilo likatili kama lina wadhifa gani.

    ReplyDelete
  11. Huyo balozi anaroho mbaya sana! Au yeye hajazaa? Tunaiomba sheria ichukue mkondo wake bila kujali hilo likatili kama lina wadhifa gani.

    ReplyDelete
  12. Huyo balozi anaroho mbaya sana! Au yeye hajazaa? Tunaiomba sheria ichukue mkondo wake bila kujali hilo likatili kama lina wadhifa gani.

    ReplyDelete
  13. Hv serikali yetu imelala au? Uweni mbwa wake na yeye then afukuzwe nchini, hafai kuwa balozi kwanini ameshindwa kuwawekea banda mbwa wake hadi kuua mtoto asie na hatia! Wadau naomba mnielekeze anakokaa huyo balozi nikaue mbwa wake mara moja!!

    ReplyDelete
  14. Realy sad!yauma sana tena sana kwa tukio kama hili kutendeka,Mungu wape nguvu wazazi wa mtoto christian.

    ReplyDelete
  15. Hivi mnangoja nini kuchukua sheria mkononi choma nyumba yake na ua yy na mijibwa yake, yaani ningekuwa napajua hapo maali pasingetosha.

    ReplyDelete
  16. No retreat, human Right First.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad