SIKU 67 ZA MIPASHO NA MATUSI BUNGENI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila kupitisha hata ibara moja kati ya 240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba.

Badala yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta “Mzee wa Kasi na Viwango” linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu likiendelea kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita zenye jumla ya Ibara 19, zinazohusu masuala yanayojenga msingi wa aina ya Muungano unaopendekezwa.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu, pendekezo ambalo limeligawa Bunge hilo vipande viwili.

Kutokana na mgawanyiko huo, kauli zenye utata, kejeli, matusi, dhihaka na ubaguzi ni mambo yaliyoshika hatamu katika mjadala wa sura hizo mbili, huku viongozi wa Bunge; Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan wakilaumiwa kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.

Mwanzoni mwa wiki hii, Mjumbe wa Bunge hilo, Ezekiah Oluoch alimshutumu Sitta kwamba ameshindwa kudhibiti nidhamu katika Bunge na kwamba ndiye chanzo cha kuondoka kwa wajumbe wapatao 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Mwenendo wa Bunge Maalumu ulikuwa na dalili zote za kuonyesha kungetokea matatizo ndani yake kutokana na mipasho ambayo ilikuwa ikitokea kwa wajumbe pamoja na lugha ambazo siyo za staha wakati wa kutengeneza kanuni,” alisema Oluoch na kuongeza:

“Kwanza matumizi ya lugha zisizo na staha, mwenyekiti anaruhusu wajumbe kuchangia hoja kwa kupeana mipasho bila kujali hoja iliyopo mezani kinyume na kanuni,” alisema Olouch.

Hata hivyo, Suluhu alisema amekuwa akiendesha Bunge hilo kwa umakini mkubwa na kwamba kila anaposikia lugha chafu amekuwa akiwabana wajumbe kwa kuwaamuru kufuta kauli au kuomba radhi kwa matamshi. “Sipendezwi na lugha chafu, kwa hiyo mojawapo ya mambo ambayo huwa najitahidi kusikiliza kwa makini kila michango inapotolewa na wajumbe bungeni ni kubaini kama wametumia lugha zisizostahili, kisha kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni zetu,” alisema Suluhu.

Alikiri kwamba wapo baadhi ya wajumbe ambao wamekuwa wakigoma au kukataa kuomba radhi na kwamba masuala yao hupelekwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo ina mamlaka ya kuchukua hatua zaidi kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. haki ya mungu nchi hii hata sielewi, inasikitisha sana siku 67 4 nonsense for God sake

    ReplyDelete
  2. yanakulaa tu!! dah nchi hii, acha tu

    ReplyDelete
  3. wizi mtupu hakuna cha bunge wala bangi

    ReplyDelete
  4. inasikitisha sana na kutia huruma kwamba nchi hii watu wengi ni masikini, lakini kuna mijitu tena viongozi ipo inachezea pesa tu bila huruma, EE h Mungu mfufue Nyerere wetu!

    ReplyDelete
  5. Katiba ilitakiwa iwe kama duka lililofilisika na linaanza upya kwa mtaji lakini sivyo,wananchi wanategemea kuanzisha upya jamii ambayo kila mtu atakua na haki sawa na heshima kama binadamu kwani ilivunjika mara baada ya kifo cha muasisi wa taifa.Lakini inaelekea sivyo na bunge la katiba limeonyesha sura halisi ya watanzania.Watu ambao hawako serious na maisha yao bado wanataka vitu vya hovyo hovyo.

    ReplyDelete
  6. hakuna dhambi kama kufanya kitu cha kuwaangamiza maskin kisa unaogopa utakosa chance next election.haiingii akili kuwa na dibaji then uandike katiba ambayo haina maudhui wa dibaji yenyewe.kuna watu wamemtukana warioba sana na kudharau mungu awape nguvu wajitambue.ma proclaim goes to our presedent maana kabla ya bunge maalumu alikuwa na rasimu zote mbili,kama aliona hazina maana bora angezivunja mapema na sio kuwaambia wajumbe wachanganye akili zao na warioba mzee wetu.naamin ana washauri wengi na wataalamu wa kutosha,na hata hao wanaopga rasimu hawakujua kama walipitisha sheria ya kutoibadilisha rasimu?mwenyekiti viwango viko wapi?kama matusi ndo yalikuwa vielezi ama vivumishi?jaman kumbuken masikin mliowaacha huko makwenu na majimboni sio kwamba hamjui bali mnaogopa kunyimwa chance next election na hapo mnasema mmetumwa na wananchi kumbe nia zao.

    ReplyDelete

Top Post Ad