SIMBA WAJUTA KUMFUKUZA KIBADENI...NI BORA MARA MIA KULIKO HUYU KOCHA MZUNGU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Simba,  Zdavko Logarusic ‘Loga’  ametimiza mechi 10 za Ligi Kuu Bara akiwa amekusanya pointi 12  lakini amezidiwa na Abdalah Kibadeni, ambaye aliinoa na timu  hiyo kwenye mzunguko wa kwanza kwani alikusanya pointi 20 katika idadi hiyo ya mechi.

Simba ikiwa chini ya Loga tayari imepoteza nafasi ya kuwania nafasi tatu za juu baada ya kufungwa Jumapili iliyopita na Azam 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hivyo kubaki nafasi ya nne na pointi zake 36.

Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 53, wakifuatiwa na Yanga (46) na Mbeya City imekamata nafasi ya tatu na pointi 45 wakiiacha Simba kwa tofauti ya pointi tisa wakati zimebakiza michezo mitatu.

Loga alikabidhiwa jukumu la kuinoa Simba, Desemba mwaka jana baada ya uongozi wa klabu hiyo kumfuta kazi Kibadeni na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo kwa madai ya kutoridhishwa na matokeo ya timu yao.

Wakati huo Simba ilikuwa ikishika nafasi ya nne ikiwa na pointi 24.

Kibadeni alidumu katika klabu hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi sita na kuiongoza kushinda mechi tano, wakitoka sare tano katika michezo 10 kabla ya kufungwa na Azam.

Mcroatia huyo aliyeanza kibarua chake kwa kishindo kwa kuiongoza Simba kushinda mabao 3-1 dhidi ya Yanga katika mechi ya kirafiki ya `Nani Mtani Jembe’, alishindwa kuhamisha mafanikio hayo katika ligi.

Tangu Januari 26, mwaka hu, Loga ameiongoza Simba kushinda mechi tatu tu, akitoka sare tatu pamoja na kufungwa mechi nne dhidi ya Mgambo Shooting (1-0),  Coastal Union SC (1-0), JKT Ruvu (2 - 3) na Azam FC 2-1.

 Logarusic alisema: “Nashangaa tunacheza sisi lakini tunafungwa, nafikiri ni kutokuwa makini, tunacheza kwa kufikiria pasi na mashuti,” alilalamika kocha huyo wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya.

Naye nahodha wa Simba, Nassor Masoud ‘Cholo’ alisema matokeo mabaya waliyoyapata kwenye kipindi hiki ni funzo kwao na sasa wajipange kwa ajili ya msimu ujao.

Cholo alisema: “Tulichokipata, kinatukumbusha kuwa, duniani kuna kupanda na kushuka, sisi tumeshateleza haina jinsi, tukubaliane tu na matokeo haya.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mpira,hauendeshwi kisiasa hakuna cha kujifunza kati ya simba na yanga,siasa na majungu ndo vinatawala,huwezi kila mara uunafukuza makocha,kwa kosa la kufungwa na mtani,mbona mkifungwa na mgambo shooting hamfukuzi kuweni na utamaduni Wa kuweka makocha wazawa,hata kwenye .timu za taifa.,igeni kwa brazili,kibaden,julio,mkwasa,wanaaweza mkiwaamini,mbona mtibwa,mbeya city,na wengine wameweza,mungu ibariki Tanzania,mungu bariki AZAM.Lucas kutoka rock city.

    ReplyDelete

Top Post Ad