Kuna wizi unafanyika kwenye mabenk kwa kweli unatia aibu na kujidhalilisha tu.
Nilikua mlimani city natoa pesa kwa ajili ya kumtumia jamaa yangu yuko Exim bank mimi niko CRDB, Basi nkatoa pesa CRDB nkaenda pale EXIM mlimani city hapohapo, Nkahudumiwa na kijana wa dirisha la kwanza toka mlango wa kuingilia.
Basi nkamkabidhi jamaa hela kama milioni tatu,akahesabu ziko sawa nkampa karatasi ya deposit akaangalia kwenye desktop yake then akanambia hiyo akaunt(ya jamaa ninaye mtumia) iko dormant jamaa hakuitumia muda mrefu, basi jamaa akanirudishia hela zangu, unfortunately muda wa kufunga bank ulikua umefika, nlikua katika watu wa mwisho kuhudumiwa.
Basi nkatoka nkampigia jamaa na kumweleza hali halisi, jamaa akakataa na kusema jana tu alitoa pesa kwenye akaunt yake, nkamwambia nakutumia kwa tigo pesa akakubali. Nkaingia ofisi za tigo pesa hapohapo mlimani city, nkaweka folen. nlipompa cashier ahesabu zimepungua kama elfu 80. nlikasirika sana, kurudi kule washafunga, basi ikala kwangu.
Ila yule jamaa nimemkariri nkikutana nae lazima nimseme na njaa za kitoto.Hivyo wakuu kosa nililofanya ni kumuamini aliponipa sikuhesabu. kuwenu makani na hawa watu.
By dikembe
Duuh! Br pole sana, hilo suala la kukosa uaminifu me binafsi huwa sipendezwi nalo kabisa, kitendo alichofanya huyo jamaa alaaniwe kabisa, sasa elfu 80 inatamfikisha wp zaidi ya kujidhalilisha na kujenga uadui na watu husio jua tabia zao, mtafute huyo br mfundishe jinsi ya kuishi na watu hapa dunian, pambafuu sana yeye
ReplyDeletepole sana mi mwenye ilinitokea sema ilikuwa sh elfu 10 tu ila iliniuma nikasema kuliko yeye achukue bora ningempa ndugu yangu alikuwa akilia shida, ila watu wa bank wanatakiwa kuwa waaminifu sana wanavyofanya sio poa, vipi hiyo elfu 80 mpaka leo hana
ReplyDeleteMimi imenitokea mara mbili,moja ilitokea standard charted mwaka 2011 na nyingine stanbic 2013 ilikuwa dola mia kila sehemu nikawa tayari nimejifunza,jitahidi kutokwenda bank dakika za mwisho na hesabu pesa zako ma
ReplyDeletera mbili kabla hujakabidhi na ikitokea ukarejeshewa usiwe mvivu kuhakiki kwani ukiwaamini unaishia kujilaumu
Pole sana ndugu yangu!mimi ilitokea CRDB tawi la Holland mana ATM ilikuwa mbovu nikaingia ndani nakumbuka ilikuwa mwaka jana yeye yule cashier ni kijana alinitolea pesa huku akiniongelesha sana maneno mengi eti sijui kaniona wapi sijui chuo,nikamwambia hapa huku ananipatia pesa matokeo yako sikuhesabu nikaondoka huku naongea nae na kuziwaka ktk handbag yangu na niliondoka hapo sikununua kitu chochote kila mpaka nafika nyumbani lakini nilipohesabu pesa maana nilichukua laki 5, nilipohesabu elfu hamsini hazikuwepo kesho yake nilirudi akasema yeye alinipatia zote na sharti la kibenki hesabu pesa zako ndipo uondoke toka hapo nilijifunza kuhesabu pesa hasa kama ATM hazifanyi kazi nikiingia ndani ya benki na hii ilisaidia tena tawi la Azikiwe nilitaka tapeliwa tena nilipohesabu nikamweleza yule dada hata waite maaskari wakanivue hata chupi ili ionekane kama nimechukua ndipo alinirudishia twenty yangu.
ReplyDeleteExim bank ya Mlimani nadhani wanayo tu iyo tabia ya wizi. mi imewahi nitokea pia nilimtuma mtu aka deposit laki 3, baada ya siku tatu nikapeleka laki 2. siku naenda kutoa kwenye ATM naoma balance ainilidhishi, nikaingia ndani kuomba statement, kwenye statement ela ipo ila kwenye account akuna. nikafatiia wakawa wananizungusha, siku nikaandika barua kwa mama mwambenja ila sikuipeleka na nikamkopi branch manager yeye nilimpa, walivoona ivo wakanipigia simu na ela ikawa imewekwa kwenye account. Exim Mlimani has to change.
ReplyDeleteKuweni makini hela kitu kingine, hakikini hela zenu kabla ya kutoka BANK, mi kuna mfanyakazi mwenzangu alishawahi tapeliwa laki 8 za mshahara, kufuatilia bank wakasema mshahara kweli uliingia, yeye kwenda kucheki kwenye account yake balance halijaongezeka, kudai bank statement inaonesha hela imeingia, lakini ilisemekana kuna mfanyakazi mmoja baada ya kuona ile account ina salio kubwa kumbe ndio alidokoa na kumtumia mwanawe ada ya chuo.
ReplyDeleteshame on you bankers na njaa zenu. Watanzania wenzangu, msifumbie macho haya mambo. Wekeni wazi hadi kwenye vyombo vya habari, msiishie tu kuandika humu kwenye mitandao kwani sio watanzania wote wanasoma. Dawa ni kuwaanika na uozo wao hawa bankers njaa.
ReplyDeleteMie nilishaibiwa hela kwa njia hio benki ya stanbic ile ya kinondoni..mara ya kwanza nikahisi alienipa kanifanyia uhuni.basi nikapotezea nikapeleka tena hela kwa mdada huyo huyo siku ya pili akanihesabia akasema laki moja haipo wakati nilihesabu hela imetimia..nilipo enda kwa maneja wa tawi kulalamika alichonijibu sitasahau ati unataka sie tukale wapi...nilipo tishia kuwenda kwa wakubwa ndio aka ahidi kufanya uchunguzi...kwa kweli hii tabia ipo sanaa..na stanbic ya kinondoni inaongoza maana kuna watu wengi wanalalamika kuhusu uhuni huo
ReplyDeleteNilishawahi kuchukua pesa NMB Kariakoo milioni moja saa kumi jioni,usiku nilipopita kuangalia balance yangu nikakuta kiasi kilichotolewa ni millioni mbili, kumbe watu wanaijua mitindo ya benki ile wakanishauri niwahi asubuhi wakifungua!Nilipofika customer service wakaniambia nisubiri baadae miliono yangu wakairudisha wakasema ni matatizo ya mtandao kumbe ningechelewa ingekuwa ndio basi.AIBU KUBWA
ReplyDeleteTatizo ni utaratibu wa nchi nzima ambao tumeukubali,wizi wizi,upendeleo kwani watu wanaajiriwa kwa kununua au ndugu ndio anakutafutia kazi kwa hiyo kuna kulindana kwenye taasisi zote and the nation as a whole is not ready to do anything about it!Kwa hiyo kuiba,kulaghai,uvivu ni moja ya sifa za Utanzania.
ReplyDeleteBenki zetu hatari haswa NMB,mfanyakazi anaweza akuambie nikuwekee milioni 10 kwenye akaunti yako uzitoe halafu unipe millioni nane,je wanazitoa wapi pesa hizo?
ReplyDelete