GARI LA GURUMO ALILO PEWA NA DIAMOND LAZUA UTATA KWENYE FAMILIA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

AMA kweli asiyekuwepo na lake halipo! Lile gari la aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi aliyefariki dunia hivi karibuni, Muhidin ‘Maalim’ Gurumo alilopewa na nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeibua utata mtupu ndani ya familia ya marehemu huyo baada ya kubainika kwamba kumbe hakupewa kadi yake

Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka ndani ya familia hiyo jambo hilo lilifahamika kufuatia mgogoro mkubwa unaoendelea kufukuta miongoni mwa wanandugu hao ambao sasa wamechangukana kutokana na mgawanyo wa mali za marehemu.
Ilijulikanaje kama hakuna kadi?
Chanzo hicho kilimtaja mtoto wa kike wa marehemu Gurumo aitwaye Mariam ambaye anataka nyumba na gari hilo aina ya Toyota FunCargo viuzwe ili watoto wagawane fedha.

“Yule binti alikwenda nyumbani kwa mama yake (mke wa mwisho wa mzee Gurumo aliyekuwa akiishi naye kwenye nyumba yake Mabibo, Dar) na kumtaka ampe kadi ya gari akidai ni la kwake na anataka kuliuza.
“Mama mtu alimwambia mwanaye kuwa baba yao hakupewa kadi hiyo siku alipokabidhiwa gari hilo.
“Hata hivyo, mama huyo alisema siku moja mzee Gurumo alimfuata Diamond alipokuwa akifanya shoo pale Coco Beach (Dar) kwa ajili ya kuulizia kadi hiyo ndipo Diamond akamwambia kwamba akitaka kadi amuulize mtu mmoja aliyesema ni kiongozi mmoja, anafanya kazi maeneo ya Posta Mpya jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa),” kilisema chanzo.


Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya Gurumo kuambiwa maneno hayo, hakutoa jibu lolote kwa mke wake kama alipewa kadi hiyo au la, lakini mama huyo hakuwahi kuiona.
Kukosekana kwa kadi hiyo kumesababisha kuendelea kuwepo kwa gari hilo, kwani kama ingekuwepo, lingeshauzwa.
Habari kutoka ndani ya kambi ya Diamond zilisema kuwa tukio la kutoa gari kwa mkongwe huyo mwanzilishi wa Bendi za  Mlimani Park Orchestra na Msondo Music Band ulikuwa ni mpango maalum wa kumpromoti msanii huyo ili aweze kung’ara zaidi katika vyombo vya habari ambao uliratibiwa na kiongozi huyo mwenye kulalamikiwa na wasanii mara kwa mara.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunatoana roho yarabiiiiiiiii kwa mali alizoaachaaa baabaa mali ya baba inanitoa roho bora nikae peemben niinusuru roho yangu mie HAYA WOTE ITIKIA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Niiinusuru miiieee yahayaaaaaaaaaaas!

      Delete
  2. hehe makubwa kiazi haya sasa kwani mambo mengi kafanya akiwa hajafa akitegemea anaenda mwisho why hakuacha wosia wa hizo mali lol! mtihani tunao binadamu tukishakufa katika familia tulizoziacha

    ReplyDelete

Top Post Ad