Nando Atangaza Kuacha Kutumia Dawa za Kulevya..Kumbe Alikuwa Teja Mkubwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Ammy Nando ameweka wazi kuwa alikuwa mmoja kati ya waathirika wa dawa za kulevya.

Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu ha 100.5 Times Fm, Nando amesema alikuwa anatumia dawa hizo za kulevya kwa muda mrefu na kwamba hadi leno ni wiki ya 16 tangu afanye uamuzi wa kuacha.

Akizungumzia sababu zilizompelekea kutumia dawa za kulevya, amesema ujana na maisha ya starehe aliyoishi vilichochea.

“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na pia pressure na watu nilokuwa nao wakati ule, na life nililoishi mimi…ni yale maisha ya kujiachia.” Amesema Nando.

Hata hivyo, Nando ameeleza kuwa ameachana na dawa za kulevya (unga) lakini bado anatumia bangi kwa hivi sasa japo amepunguza idadi.

“kuhusu bangi…sisi tunaitaga stock, natumia moja au mbili kwa siku.”

Ameongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu wenye kibali cha kuvuta bangi  kwa maelezo ya daktari kuwa anafanya hivyo kwa lengo la kuacha kutumia unga.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kumbe bigi buraza wanachukuwa mpaka mateja, duh halafu watu wanayapigia kura!!! aiseee

    ReplyDelete
  2. This time badala ya kuua lulu atakufa yeye maana hiyo no ya nan do ndo type yake,rip uncle JJ,

    ReplyDelete
  3. big borther ni mahali pa mafunzo huoni amejifunza

    ReplyDelete
  4. alikuwa teja anaonekana hata ongea yake we humuoni, haongei maneno yakasimama hovyo hovyo tu

    ReplyDelete

Top Post Ad