Timbwili lazuka baada ya Jaji Werema kumfananisha Mbunge Kafulila na TUMBILI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, ameteleza ulimi tena na mara hii amejikuta akimuita Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) tumbili.

Kabla ya kutoa kauli hiyo, Werema alikuwa akitoa ufafanuzi wa mwongozo ulioombwa na Kafulila, kuhusu fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambazo zimelipwa kwa kampuni ya PAP, inayomiliki mitambo ya kampuni ya umeme ya Independent Power Tanzania Limited(IPTL).

Werema alisema fedha hizo si za Serikali, kama inavyodaiwa na Kafulila, kwa kuwa fedha za Serikali, hazikai katika akaunti hiyo.

Alifafanua kuwa taarifa zinazotolewa, zinapotosha umma kuwa serikali imetoa fedha kuilipa IPTL, wakati ukweli ni kuwa fedha hizo ziliwekwa katika akaunti hiyo, kutokana na misuguano baina ya wanahisa wawili, waliokuwa wamiliki wa IPTL

Werema alibainisha kuwa mmoja wa wanahisa hao, alikuwa akitaka IPTL ifilisiwe, huku mwingine akipinga jambo hilo mpaka walipouza hisa zao na kumaliza mgogoro huo, ambapo Mahakama iliruhusu mali za kampuni hizo,  apewe mwanahisa mpya, PAP.

Werema alisema kuna watu walileta bungeni  vipeperushi, wakidai ni ushahidi kuhusu utoaji wa fedha hizo za akaunti ya Escrow na kuhusisha na rushwa.

“Kafulila ni miongoni mwa  wanaoeneza taarifa potofu…kama ni tuhuma au kuna rushwa, itakuja kujulikana, tusubiri uchunguzi wa vyombo husika,” alisema.

Wakati akizungumza, Werema alitumia mfano wa kabila la Wanyankole, aliosema kuwa wana usemi unaosema kwamba ‘Tumbili hawezi kuamua kesi ya msituni’.

Kabla ya kufafanua maana ya msemo huo, Kafulila bila kuwasha kipaza sauti, alikuwa akipiga kelele kumuita Werema kuwa ni mtuhumiwa, hivyo atangaze maslahi yake.
“Naomba nisikilize, hata kama ni mtuhumiwa, nina fursa ya kusikilizwa …nisikilize wewe tumbili,” alijikuta akisema Werema.

Baada ya kusema hivyo, Kafulila hakukubali ;na yeye bila kuwasha kipaza sauti, alisema: “Wewe (Werema) ni mwizi tu.”

Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan ‘Zungu’ alimuomba Jaji Werema, kukaa chini ili atoe ufafanuzi, huku Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) na Kafulila wakitaka kuzungumza.

Zungu alisema kwa kuwa Bunge, lilishaamua kuwa suala hilo, lipelekwe Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ni vyema kama Kafulila ana ushahidi wowote, apeleke huko.

Baada ya kutoa mwongozo huo, ambao ulisitisha malumbano, Mwenyekiti Zungu alisitisha shughuli za Bunge mpaka jioni na kuondoka, huku akisindikizwa na makatibu wa Bunge na wapambe kama kawaida.

Hatua ya Mwenyekiti wa Bunge kuondoka katika ukumbi, baada ya kusitisha shughuli za Bunge, ilimpa fursa Jaji Werema kuweka sawa makabrasha yake na kutoka katika kiti chake, ambapo alionekana kama vile anakwenda kumkabili Kafulila.

Wakati hilo likitokea, Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester
Kasulumbayi (Chadema), alihama katika kiti chake na kukimbilia alipokuwa amekaa Kafulila.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya mawaziri  walimzunguka Jaji Werema, kabla hajamfikia Kafulila na Kasulumbayi.

Mawaziri hao ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha Rose Migiro na Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Abdullah Juma Abdullah Saadalla.

Nje ya Bunge, Kafulila na Mnyika waliitisha mkutano na waandishi wa habari, ambapo walidai kuwa na ushahidi wa kutuhumu baadhi ya mawaziri, kusema uongo bungeni kuhusu fedha hizo za Escrow.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dizaini kama tumbili kweli vimacho vyake....lkn tumbili huyu uwezekano anajitambua....ana darubini kali...atoe ushahidi ili ijulikane kweli kuwa werema ni muongo....uongo wa kwanza wa werema ni kumwita kafulila tumbili wakati si kweli ni jazba zake....ajisafishe kuhusu tuhuma hizo zinazomkabili

    ReplyDelete
  2. Hako kazee n kaizi sana hata machoni mwake anaonekana n kapigaji 2 akana lolote kameishiwa mbinu

    ReplyDelete
  3. Muizi mkubwa! Kazi kuita watu tumbili ngojeni kumamae zao ipo siku zita watokea pwana

    ReplyDelete
  4. kumamae wabunge wote

    ReplyDelete
  5. Mhs Kafulila na Mh Myika yaumbueni hayo majambazi, bila nyinyi yatabaki kutafuna tu! big up to both of u!

    ReplyDelete
  6. maskini huo ndio utetezi wake werema hana cha kujitetea zaidi yahapo

    ReplyDelete
  7. yaah eti linaitwa jaji kuiaibisha professinal ye2 jaji unakuwa na kauli chafu na kusahau maadili ya proffessinal ya law mxstyuuuuuuuuu......... Jizi kubwa gogo mfulila show him he z gd 4 section 265 of the penal code Cap 16 RE 2002!

    ReplyDelete
  8. mijitu kama hii china wana wanapiga risasi tuu kuma nyoko zao viongozi wa ccm woote ni wezi tuu kuma nina zao!yeye mbona limefanana na sokwe msura kama uvungu wa pumbu!mwizi mkubwa!

    ReplyDelete
  9. Hivi kafulila huwa ana meno? Maana naona kweli kafanana na tumbili teh teh teh.

    ReplyDelete

Top Post Ad