RAY C Alitamani Penzi la Babu Kizee…Adai Kuchoshwa na Vijana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu, na kama ikitokea basi atamtaka kuwa na miaka kuanzia 60.

Akizungumza katika kipindi cha ‘The Sporah Show’, Ray C alisema anahitaji wanaume wa umri mkubwa, kwa kuwa wanajua wanachokifanya, na kukiri kwamba vijana walichangia katika kurudisha nyuma maisha yake.

Msanii huyo ambaye kwa sasa ameanzisha asasi yake ya kupambana na dawa za kulevya, kutokana na yeye kuwa mmoja wa waathirika wa dawa hizo, alisema katika moja ya mambo anayoyajutia ni kuwa na mahusiano na vijana, jambo ambalo hataki kukumbuka walichomfanyia hadi kudhalilika mbele ya jamii.

Hata hivyo, alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi kutowatenga watoto wao ambao wamejidumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya na badala yake, wawakumbatie na kuwaonyesha njia kama mama yake alivyofanya na kurudia hali yake ya kawaida.
Kuhusu kurudi kwenye muziki, Ray C alisema yupo mbioni na tayari ameshatengeneza nyimbo kadhaa, ambapo hivi sasa atakuwa akiimba miondoko tofauti tofauti, ikiwemo taarabu.
Katika kurudi kwenye muziki, jambo la kwanza alisema anatarajia kupunguza mwili wake kwa kufanya mazoezi, kwani hata daktari wake alishamwambia anatakiwa kupungua kutokana na umri wake kutoendana na kilo alizonazo.
Alipoulizwa mwanamuziki ambaye kwa sasa anamkubali Bongo, Ray C alisema wa kwanza ni AT akifuatiwa na Recho kutoka Jumba la Kukuza Vipaji (THT).
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hujasema kweli yako mamdogo

    ReplyDelete
  2. Dada uokoke sasa achana na dunia hao vikongwe wako unaowataka watakuua kwan wanandoa zao uspende kuchezewa nao kuwa na kjana wako mwaminifu km mm ujenge familia takatifu.Jack mzalendo

    ReplyDelete
  3. Dada uokoke sasa achana na dunia hao vikongwe wako unaowataka watakuua kwan wanandoa zao uspende kuchezewa nao kuwa na kjana wako mwaminifu km mm ujenge familia takatifu.Jack mzalendo

    ReplyDelete
  4. dada mrudie mungu wako achana na izo mambo kwan mung kakunusulu chagua mmoja mfunge ndoa

    ReplyDelete
  5. umelewa ww dada ujui hao wababu wana wake zao, labda uchukue wajane

    ReplyDelete
  6. Mfate mzee mutalemwa

    ReplyDelete
  7. Babu yupi anataka PEPSI MIRINDA??? Labda utapata wenye virus vya HIV

    ReplyDelete

Top Post Ad