Taarifa mpya ya Luis Suarez, hii ndio adhabu atakayopata akikutwa na hatia ya kumn’gata mchezaji mwenzake.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mchezaji wa Uruguay Luis Suarez atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa muda mrefu kucheza mechi zikiwemo za Kombe la dunia ikiwa atakutwa na hatia ya kumng’ata mchezaji mwenzake wa Italia Giorgio Chiellini.
Shirikisho la soka duniani limeanzisha uchunguzi dhidi ya mchezaji huyo  baada ya kuonekana akimng’ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao ya kombe la dunia.

Chiellini amedai Suarez amemng’ata katika bega lake la kushoto lakini Suarez amejitetea kuwa mchezaji huyo alijigonga kwake.
Refari wa mechi hiyo hakuchukua hatua yoyote dhidi ya Suarez.
Ikiwa atapatikana na hatia, Suarez huenda akazuiwa kucheza mechi 24 au kwa miaka miwili.
Suarez mwenyewe tayari amejitetea katika vyombo vya habari nchini Uruguay.
Suarez anasema Kuna mambo fulani ambayo hutokea uwanjani na hadhani ni vyema kuanza kuzua kashfa kutokana na mambo kama hayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ili jamaa inabidi likapimwe akili, limejaliwa talent nzuri lakini kichwani maji matupu!

    ReplyDelete

Top Post Ad