Barrick Yamfukuza Kazi Kijana kwa Kumtongoza Mwanamke wa Kihindi.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ni tukio la aina yake lililojaa kila aina ya ubaguzi wa rangi, ni week iliyopita kijana aliyekuwa akifanya kazi ktk mgodi wa Bulyanhulu wa Barrick, amefukuzwa kazi baada ya kuonyesha hisia zake kwa binti wa kihindi raia wa south africa, ambaye naye ni expat wa mgodi ule,walipeana namba za simu, kijana wa watu akatupa ndoana kujaribu bahati yake, mambo yakamgeuka,binti mbaguzi kashtaki kwa makaburu wa mgodini, kesi ikaitishwa, hukumu ikatoka kuwa kavunja sheria kwa kumnyanyasa kimapenzi, kazi ikaisha, ajabu ni kuwa weusi huwa wanatongozana lakini hakuna kesi, wala kufukuzwa kazi, lakini baada ya mweusi kumtongoza mweupe, kibao kikageuka kuwa ni sexual harassment, tukio hili limepandisha hasira watu, kwa nini mtu abaguliwe ndani ya ardhi yake? na wageni tu? tena wenye njaa waliokuja kujistiri kwetu? nimeongea kwenye simu na huyu kijana,wk ijayo naelekea Bulyanhulu ili kuonana naye nimshawishi aipeleke mahakamani kampuni hii ya kitapeli,i nayokumbatiwa na watawala wa ccm wasioipenda Tanzania hata kidogo, Mungu bariki Taifa letu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya ni mambo yanayowakuta majamaaa wengi katika Nchi za watu. Ukijipendekeza
    kidogo tu unaambiwa eti ni sexual harassment. Lakini wao kwa wao aahh wanashikana wanapigana mabusu tena mbele ya meneja wao. Poleni sana wa Tanzania kwa hilo suala kutokea ndani ya Nchi yenu msikubali hakikisheni mnakula sambamba na hiyo kampuni. Haiwezekani wabongo tunyanyaswe katika Nchi za watu na tunyanyaswe katika Nchi yetu pia. Nooooooooooooo haiwezekani.

    ReplyDelete
  2. Na actually sio tu sexual harassment. Utaambiwa sijui ni unprofessional, sijui ni against working ethics na kadhalika. Ilimuradi tu waishie kukukomesha. Lakini cha ajabu hao hao majamaaa wakiwataka dada zetu aaahhh utakuta wanawashikashika wanawachezea wanavyotaka na dada zetu walivyokuwa wajinga na malimbukeni wanakubali. Sasa sijui ni kwa sababu ya unyonge????? Anyway hiyo ni experience yangu ya hayo mambo katika hizi nchi za watu. Sasa nashangaaa kwa nini leo hii yaruhusiwe kutokea katika ardhi yetu wenyewe. Nooooo haiwezekani huyo kijana ni lazima arudishwe kazini na ikiwezekana iitishwe petition. Watu watanzania wenye uchungu na nchi yao itabidi wa sign hiyo petition. Tusikubali kuonewa katika Nchi yetu na hao wabaguzi. Aliyekuwa Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere aliisha yakataa mambo hayo. Sasa sijui kuhusu viongozi wa leo wanasemaje.

    ReplyDelete
  3. Waache huo ubaguz mbna bado wanathamin xana hao wa2 weupe kulko mzawa! wabadilike bana na c kunyanyaxana khvyo,

    ReplyDelete
  4. Sina uhakika ni yupi aliepotosha ukweli kati ya Muathirika au Admin, kwanza kabisa sio kwamba najaribu kutetea Barrick ila napenda tujadili hili kwa njia inayoelezea kadhia hiyo ilivyokuwa, kwanza si kweli bwana huyo amefukuzwa kazi kwa kosa la kutongoza la hasha bali kwa kosa la kutumia mawasiliano ya internet kutuma pornographic material, kwa barrick ina sheria zake kuhusu matumizi ya internet zipo nyingi ikiwemo hiyo inayokataza mambo ya porn. sasa basi jamaa yetu alikuwa na mawasiliano na dada yetu mtanzania mwenzetu ambae alikuwa site nyingine ilikuwa kama bahati mbaya alimtumia mtu ambae hakumkusudia kumtumia ambaye ndio huyo mgeni baada ya muda alimpigia simu kutaka kujua kama aliziona hizo picha yule alie mkusudia jibu lilipokuwa tofauti akarudi kucheck ndio kukuta ametuma kwa huyo hivyo alikwenda kumfuata huyo mdada raia wa kigeni kumuelezea kuwa hakukusudia kumtumia yeye lakini mgeni huyo alikuwa tayari kesha lisogeza mbele huo ndio mkasa ulivyo kuwa kwa kifupi...

    ReplyDelete
  5. Watanzania naomba tusilete suala la rangi ya mtu katika mambo yanahusu uamuzi wa mtu hayo mambo ya mtu wenyewe anavyoamua kufanya halihusu rangi ya mtu. Ukijiheshimu watu watakuheshimu na hili linatokana na uamuzi wa mtu mwenyewe ukiona katika mitandao baadhi ya dada zetu wameingia kwa fujo wanaona kama sehemu ya kuziweka picha zao za uchi na kuweka mambo ambayo hayaendani na maadili yetu, je wenzetu watanzania hao mnaowaita wahindi mnawaona wanaweka hizo picha zao mitandaoni sasa hayo ni maamuzi ya mtu binafsi kwahiyo usitake kulazimisha mbona wao wanatongoza wanawake wetu hayo ni maamuzi ya mtu binafsi si kwasababu ya rangi au dini yake.

    ReplyDelete
  6. Kwa Hilo linatakiwa kuuliza pande zote mbili,lakini ninavyoelewa ukiwa mgodini ndani suala la ngono Ni ishu ya kufukuzwa kazi Ata kwa hao wageni....japo kampuni hii ina chembe za ukandamizaji angalia wafanyakazi wa bulyanhulu waliofukuzwa kazi 2007 wanavyotaabika kwa maisha magumu na wengine kuendelea kupoteza maisha kutokana na athari walizopata mgodini....yoote yaangaliwe. Hii ya huyu jamaa sijuiii..

    ReplyDelete
  7. Inasikitisha sana pamoja na haya yote kutokea inawezekana ikawa na ukweli kavunja sheria za kazini lkn jmn watanzania wananyanyaswa kwa uroho wa fedha za viongozi wetu.. Hao wageni wanaringa coz wanakula na viongozi wa ngazi za juu.asee

    ReplyDelete
  8. watanzania wananyanyaswa sana,wanalipwa mishahara midogo ukilinganisha nao wanaitwa ma expert ambao wanakuja hawajui kazi,wanafundiswa na watanzania,chakushangaza watanzania wanalipwa kidogo kuliko ao,kuna unyanyasaji sana barrick

    ReplyDelete
  9. na sio migodini tuu nenda VIP LODGE GRUMET SINGITA ipo Serengeti, yaani hata askari wa ulinzi wamewekwa makaburu, fujo tupu! wakaburu siwapendi hata kidogo wanyanyasaji na wabaguzi sana.. maliasili zetu wanafaidi wao.

    ReplyDelete
  10. kama ni ubaguzi kwa sababu au ni mhidi wa south africa au wenyewe ni bora sio kweli kwamba ni zaidi yetu sisi watanzania .watu wanawababikia tu huko mbona hapa kwao wanapata shida tu wanazalishwa na watu weusi especially wanabaika wageni wa kiafrika na wengine ni madada poa tu .na wengine wanafagia mabara bara hapa .kwao hapa ni wabaguzi wakubwa kwa wageni kupata kazi .ukienda kwenye mabenki yao kama fnb wanaweka sheria ngumu kwa wageni kufungua account lakini bado wanakuja huko kwetu na kufungua mabenki na kutafuta wateja ni unafiki wao hao wasouth africa .

    ReplyDelete
  11. Watanzania tunatakiwa kuwa na umoja, siyo watu mnaongea tu brabra za mdomoni tu, hapo ilitakiwa watu wote hamna kutinga hadi jamaa arudishwe kazini, tumeona nchi nyingi za Africa watu wameamka sana hakuna kutoralet rangi hata kidogo, sema wabongo mkiona mtu kapata issue kama hiyo mnakaa juu mnamuachia jamaa yeye peke yake mnatakiwa muamke ndugu zangu

    ReplyDelete

Top Post Ad