Chadema: Ofisi ya Msajili inatumiwa wa Vyama Inatumiwa Vibaya na Wasaliti wa Chama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mvutano mpya umeibuka baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumvaa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kikidai ofisi yake inatumiwa na wasaliti wa chama hicho.

Pia, chama hicho kimemtaka Jaji Mutungi ajitokeze hadharani kubainisha iwapo yeye ndiye aliyemtuma msaidizi wake, Sistyl Nyahoza kutangaza kuwa mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa hawana sifa ya kugombea uongozi ndani ya chama hicho kutokana na kuzuiwa na katiba ya Chadema.

Jana, Nyahoza alikaririwa na vyombo vya habari akisema Mbowe na Dk Slaa hawana sifa za kugombea uongozi wa chama hicho kutokana na katiba ya chama chao kuwabana.

Alibanisha kuwa kipengele cha ukomo wa mgombea katika katiba yao ya mwaka 2006 kiliondolewa kinyemela bila idhini ya mkutano mkuu.

Nyahoza alisema katiba ya Chadema ya mwaka 2004, ilikuwa na kipengele cha ukomo wa madaraka kuwa kiongozi aliyeongoza vipindi viwili vya miaka mitano mitano, hawezi kuwania tena nafasi hiyo.

Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema Jaji Mutungi hana mamlaka ya kubaini sifa za viongozi wa chama hicho, bali wenye mamlaka hayo ni wanachama wa chama hicho pekee.

Mnyika alisema mwaka 2006, katiba ya Chadema haikurekebishwa, bali iliundwa upya na kuridhiwa na mkutano mkuu wa chama na kwamba Agosti 13, 2006 ilizinduliwa na nyaraka zote alikabidhiwa Msajili wa Vyama wa wakati huo, John Tendwa.

Katika uzinduzi huo wa katiba pamoja na bendera mpya ya Chadema, Tendwa alikimwagia sifa chama hicho kwa kuonyesha mwelekeo na mwenendo mzuri na kuvishauri vyama vingine viungane nacho kuunda chama cha upinzani chenye nguvu nchini.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Mbowe alikaririwa na gazeti hili Agosti 15, 2013 akisema yalikuwa yanalenga kuimarisha mapambano ya kisiasa ya chama hicho.

Mnyika alisema: “Mkutano mkuu wa chama uliipitisha Katiba hiyo baada ya mchakato mrefu wa kukusanya maoni kutoka kwa mabaraza ya wilaya na majimbo. Hatukurekebisha katiba kama inavyoidaiwa. Ni makubaliano ya wanachama wote ambao waliafikiana na mambo yaliyotakiwa kuwamo.”

Alisema katika mchakato huo kulikuwa na makubaliano na mabishano katika baadhi ya masuala lakini suala la ukomo wa uongozi liliafikiwa na wanachama wote bila tatizo na kupitishwa kuingia katika katiba na Ofisi ya Msajili ilipelekewa fomu ya marekebisho pamoja na katiba mpya kama sheria inavyotaka... “Kama wameipoteza waseme tuwapatie katiba wairejee.”

“Tunachomtaka Mutungi ni kuheshimu katiba ya chama na kuwaheshimu wanachama wa Chadema na ayapuuze madai ya wasaliti wachache. Kama vipi asubiri aone uamuzi wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ubainishe kama katiba ilivunjwa,” alisema Mnyika.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ccm ina haha,mara chadema ni cha udini,ukanda,ugaidi na sasa wanatumia kete ya mwisho ya katiba. Fyuuu Ushuzi mtupu.

    ReplyDelete
  2. CCM wameshikwa pabaya sana hawana pa kushika sasa wanakimbilia kwa msajili wa vyama

    ReplyDelete
  3. CCM wameshikwa pabaya sana hawana pa kushika sasa wanakimbilia kwa msajili wa vyama

    ReplyDelete
  4. CCM wameshikwa pabaya sana hawana pa kushika sasa wanakimbilia kwa msajili wa vyama

    ReplyDelete
  5. CCM wameshikwa pabaya sana hawana pa kushika sasa wanakimbilia kwa msajili wa vyama

    ReplyDelete
  6. CCM wameshikwa pabaya sana hawana pa kushika sasa wanakimbilia kwa msajili wa vyama

    ReplyDelete
  7. chezea Chadema wewe, huyu msajili hana maana yeyote, utaichaguliaje wanafamilia baba wakuishi naye? jamaa lile lishaanza kuwa kama lile tendwa!! haya majamaa mimi nayaombeaga mabaya kweli sababu hayaitakii hii nchi mema, yanafikiria matumbo yao tu!

    ReplyDelete

Top Post Ad