Lowassa Aweka Wazi Mali zake Aseme yeye sio Tajiri Bali ni Mfugaji tu Monduli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema madai kwamba yeye ni tajiri hayana ukweli wowote. Amesema yeye ni mfugaji na anamiliki ng’ombe zaidi ya 800 katika Jimbo la Monduli, mkoani Arusha.

Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake wiki iliyopita mjini Dodoma.

 “Haya madai hayana hata chembe ya ukweli hata kidogo, isipokuwa mimi nadhani wananitakia mema kwa sababu ukiona jumba zuri wanasema la Lowassa, gari nzuri la Lowassa, kitu chochote kizuri wanasema cha Lowassa,” alisema na kuongeza:

“Wamesema uongo mwingi sana, mimi nasema tu nilichopata nimepata na sina utajiri kiasi hicho, lakini si mbadhirifu wa haki zangu ninazopata kama mshahara na haki nyingine.”

Alipotakiwa kutaja mali anazomiliki, Lowassa alisema: “Mimi ni mfugaji, nina ng’ombe zaidi ya 800 jimboni kwangu Monduli.”

Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli, alisema madai kwamba anamiliki utajiri uliopindukia yalianza kabla hajajiuzulu uwaziri mkuu na ilielezwa kuwa “maduka fulani” ni yake.

Alibainisha kuwa hata kampuni ya Alphatel ambayo wanamiliki kwenye familia yake iliwahi kuhusishwa na jengo kubwa lililojengwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia wilayani Kinondoni, Dar es Salaam likiitwa Alpha.

“Ikaonekana ni jengo langu, kule Mbezi kuna rafiki yangu mmoja walienda watu wakasema hii nyumba ya Lowassa. Yule bwana alitoka na bastola akawakimbiza. Mimi sina nyumba maeneo hayo,” alisema Lowassa.

Bomu la ajira

Akitaja njia za kutegua ‘bomu la ajira’ kwa vijana ambalo amekuwa akisema liko mbioni kupasuka, Lowassa alitaja maeneo mawili ambayo yanapaswa kutazamwa ili kuzalisha ajira nyingi mpya.

Alitaja kilimo akisema kinachukua watu wengi nchini. Alisema kinapaswa kutengenezewa mazingira ili vijana wanaomaliza chuo kikuu wawe tayari kuishi kwenye mazingira ya kilimo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. usituwekee story za kijinga wewe na lowasa wako,kawadanganye wamasai monduli.

    ReplyDelete
  2. Waandishi nanyi kwa kukuza mambo hamjambo, mali mnazo sema kaweka hadharani ziko wapi?

    ReplyDelete
  3. Bilionea lowasa endelea kujidanganya mwenyewe

    ReplyDelete
  4. Halafu acheni kufanya taifa la wajinga!?! Hv kwa kipi alichosema hadi utuambie kuwa ameweka hadharani mali zake? Acha zako admin

    ReplyDelete
  5. Huyu mtu kapania kuwa rais Wa nchi,duuu Si muwaachie na wengine Jamani ?mshakula vya kutosha

    ReplyDelete
  6. Lowasa wewe mwizi tena jambazi kabisa utajiri wa ngombe una v8 5?misafara yako huwa tunairatibu usituletee ujinga wako chukua tyme

    ReplyDelete
  7. Huyu mwandishi ni mang'aa kweli

    ReplyDelete
  8. Hahahaaaaa anataka kufia madarakani siahangaikie afya yake huko apumzike.hayamchagueni muone kazi huyu wasasa cha mtoto tutabaki vichwa tu chezea ubinafsi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa nini vjana wengi wapo sawa bado mnaweka hao mastaafuu

      Delete

Top Post Ad