Hausigeli Adaiwa Kumuua Mwajiri Wake kwa Kumchoma Kisu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Asha Juma(24), ameuawa kwa kuchomwa kisu na mfanyakazi wake wa ndani.

Tukio hilo limetokea jana saa 4:00 asubuhi eneo la Sabasaba katika kata ya Utemini mjini Singida.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema mauti yalimfika karani huyo mara baada ya kuchomwa kisu sehemu ya titi la kulia na mfanyakazi huyo wa ndani aitwaye Valetina Kerenge(17).
Msichana huyo ambaye ni mwenyeji wa mkoani Mwanza wilayani Ukerewe,  inasadikiwa alilifanya tukio hilo wakiwa ndani na baada ya hapo alipata kiwewe na kukimbilia nje ya nyumba aliyokuwa akikaa na kwenda kwa majirani kuomba msaada.
Inasemekana wakati juhudi za majirani za kunusuru uhai wake zikifanyika ili kumuwahisha hospitali kwa matibabu, ghafla marehemu huyo alianguka chini na kufariki papo hapo.

“Imesikitisha maana chanzo halisi hakijajulikana, maana msichana huyu alipoona mambo siyo alikimbia,” alisema Kamanda Kamwela.
Kamanda alisema tayari msako mkali wa polisi ulifanikisha kumpata majira ya saa 8 mchana akiwa katika harakati za kutoroka maeneo ya uwanja wa ndege.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi, na baada ya kuchunguza ndugu wa marehemu watakabidhiwa kwa taratibu za kuusafirisha mwili huo kuelekea mkoani Shinyanga kwa mazishi.
Jeshi la polisi linamshikilia msichana huyo kwa ajili ya mahojiano.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Iwe ni fundisho kwa nyie wanyanyasaji wa ma maids. Acheni mara moja mtauwawa muishe. Oo

    ReplyDelete
  2. Pole sana ndugu wa marehemu, lkn iwe fundisho kwa wadada mnao penda sitarehe za nyumbani mnatafuta mahausigeli,kupika apike housegeli, kudeki chumbani adeki housegeli,kutandika atandike housegeli,mkome wakina mama ndiomana ukinitafutia housi geli aliye kudhidi shep lzm nimgegedue,acheni ubishoooooo! BY JOEL J.A.M.

    ReplyDelete
  3. Nina house girl kwangu. Nagombana na mke wangu kwa kumuona anamfokea huyo msichana karibu kila cku na sometime kwa kosa la kijinga kabisa au ubinadam tu hakuna alie kamili.
    Binafsi nachukia sana kuona wasichana wa kazi wananyanyasika kwa vile ni maskini na wana shida.
    Namdhibiti mke wangu but nikisafiri tu house girl wanaondoka huku nyuma kwa masimamgo na mateso.
    Ndugu hawa watu wanahitaji heshima pia. Upendo na uhuru.
    Msichana aamke saa 11 asubuhi alale saa5 usiku ingekuwa ww utaweza?
    Halafu hakuna likizo wala wkend. Sasa sikilizeni kina mama hao wasichana wanakua na wanamahitaji kama yenu ya unyumba. Muwe munawaachia muda kidogo wakapunguze nanihino wanakojua. Vinginevyo mtaporwa waume zenu siku zote.
    Ndio mnadhani wenzenu hawataki utamu?

    ReplyDelete
  4. Wambie hao mamama yamekuwa yapo yapo2

    ReplyDelete
  5. Poleni wafiwa , pia ni fundisho kwa madada wavivu kazi kidgo tu house gal, uvivu umewajaa na kuridhika na vijisent vya mboga, pumbafuuu wakubwa!!

    ReplyDelete

Top Post Ad