January Makamba Akomalia Urais 2015..Awashangaa Wanaombeza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema hatakatishwa tamaa na hatorudi nyuma katika harakati zake anazoziita za fikra mpya na mawazo mapya za kushika dola na kwamba wazee wakae kando. 

Hata hivyo, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM) amewashukuru watu wanaozungumzia nia yake ya kuwania urais mwaka 2015 na kutengeneza mjadala unaoendelea nchini, jambo ambalo alisema linaashiria kuwa dhamira yake imeeleweka.

Akiwa London nchini Uingereza mapema mwezi huu, Makamba alitangaza nia hiyo na kusema amefikia uamuzi huo kwa asilimia 90 lakini bado asilimia 10 katika baadhi ya mambo anayoendelea kuyatafakari, yakiwamo ya kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini na viongozi waliopita ili apate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hilo.

Julai 9, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, ambaye anamzidi januari kwa miaka 24, alisema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Soni, Bumbuli mkoani Tanga kuwa Makamba anataka mambo makubwa, lakini hajamshirikisha.

Rais Kikwete alimtaka Makamba “asilazimishe” kwa kuwa wakati ukifika atapata kile anachokitaka. “Mie hajaniambia na mie nasikia,” alisema Kikwete.
Akizungumzia na gazeti la Mwananchi jana kuhusu kauli ya Rais Kikwete, Makamba alisema: “Ni kweli sijamwambia. Siku itakapofika yeye ni mwamuzi na mwenyekiti wa chama hivyo nitamweleza. Sitaki kumkwaza kwani na yeye ni wale waliopo katika kundi la asilimia kumi,” alisema.

“Zama za kizazi kipya za kutatua changamoto kwa kipindi cha miaka 30 hadi 50 ijayo zimewadia. Nitahakikisha mabadiliko ya haraka katika ardhi ya Tanzania kwani inawezekana rasilimali za kutosha zipo kilichobaki ni kuweka nidhamu katika nyanja zote.”

Aliwashangaa wanaombeza akisema kuwa hawamkatishi tamaa kwa hilo.

Quote of The Day:
“You can't depend on your eyes when your imagination is out of focus.” 
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kaza Boot Broo

    ReplyDelete
  2. Ucje ukawa Ni wale wale waliokunywa uji WA mgonjwa!!!!???

    ReplyDelete
  3. Mh haya endeleeni kubwabwaja maana yasasa tu yanachosha turudie kosa tena eeh???maana tuvipofu

    ReplyDelete

Top Post Ad