Maskini Yule Mwanafunzi wa Chuo Aliyechomwa Moto Kwa Kuzaniwa Mwizi Afariki Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College – RUCO), amefariki dunia baada ya kushambuliwa kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira akidhaniwa kuwa mwizi.

Tukio hilo lilitokea Juni 24, 2014, majira ya saa 5 usiku ambapo inadaiwa kuwa Daniel alikuwa ametoka kuangalia michuano ya Kombe la Dunia, akawa anatafuta chakula cha jioni ambapo alipofika kwenye mgahawa mmoja ambao ulikuwa umefungwa, aliingia ndani ambapo binti aliyekuwa amelala ndani ya mgahawa huo, alianza kupiga kelele za mwizi zilizowakusanya wananchi wenye hasira kali.

Wananchi hao walianza kumshambulia Daniel wakiongozwa na mlinzi mmoja wa jamii ya Kimasai, baada ya kuzidiwa na kichapo wananchi hao walimmwagia mafuta ya taa na kumchoma moto kisha wote wakatoweka.

Mwanafunzi huyo aliokolewa na madereva bodaboda ambao walizima moto na kumkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa lakini siku kadhaa baadaye alifariki dunia.

Mwili wa marehemu umeagwa mapema leo katika hospitali hiyo tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Jumatano.
Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College – RUCO) enzi za uhai wake.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah!!R.I.P~Daniel

    ReplyDelete
  2. DAHHH !!! BT RIP D

    ReplyDelete
  3. Uyo mfanyakaz wa mgahawa anatakiwa kufungwa pamoja na uyo mlinzi

    ReplyDelete

Top Post Ad