Maximo Aanza kazi Yanga Kwa Mikwara Atangaza Week Nne za Hatari, Tegete Apewa Majukumu ya Taifa Stars

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KOCHA Mkuu mpya wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, jana alianza kazi yake kwa mkwara mzito huku kila aliyehudhuria akionyesha kutikisa kichwa kuikubali.

Maximo majira ya saa mbili kamili asubuhi alikwishatua kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam na kuanza rasmi mazoezi na timu hiyo ya Jangwani na kuwakusanya tena wachezaji wake saa tisa kamili kwenye Uwanja wa Bandari Tandika kwa mazoezi ya takribani saa mbili.

Maximo ambaye amekuwa akifanya mambo yake kisasa, alianza kama kawaida yake huku akiwasimamia wachezaji wake kunyoosha viungo na baada ya hapo kuanza kuwakimbiza.
Wachezaji wa Yanga ambao wengi walikuwa wametoka kwenye mapumziko, walikimbizwa kwa umbali wa kilomita 1.5 mara mbili kwenda na kurudi huku kocha huyo akiungana nao akiwa na kocha wa vijana, Salvatory Edward.

Maximo alionyesha kuwa yupo fiti pamoja na kwamba umri umeenda baada ya kuanza na wachezaji hao na kumaliza nao mbio bila kupumzika sehemu yoyote ambapo walitumia dakika 30.
Mara baada ya kumaliza kukimbia, wachezaji wa Yanga walitakiwa kupumzika kwa kunywa maji na kunyoosha viungo na kuanza zoezi la kuruka koni na kukimbia mbio fupi ambazo zilichukua dakika 30, msimamizi akiwa ni kocha msaidizi, Leonardo Neiva.

Kama ilivyo kawaida yake, Maximo aliendelea na utani wake huku akichombeza kwa maneno ya Kiswahili; tupo pamoja, harakaharaka, ongeza mwendo, usichoke na mengine mengi.
Baada ya kumaliza kuruka koni, Maximo alionyesha kuridhika na kuwaita pamoja na viongozi wengine waliokuwepo uwanjani hapo na kuzungumza nao.

Baada ya mazungumzo kocha huyo aliwakusanya wote na kuomba dua na kutawanyika ambapo aliwapa ruhusu ya kuzungumza na waandishi, lakini yeye akapanda prado lake na kutimka.
Hata hivyo, saa tisa alasiri kocha huyo alilianzisha tena na mastaa wake kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari, Temeke ambapo alianza kwa kuwazungusha uwanja raundi tatu huku kukukiwa na mashabiki kibao.

Mashabiki hao walishuhudia mazoezi mazuri huku kocha huyo akiwataka wachezaji wake kufanya kila kitu kwa uhakika.
Mashabiki waliofurika uwanjani hapo walionekana kushangilia kwa nguvu kubwa kila Mbrazili Coutinho alipokuwa akigusa mpira na wakati Maximo alipokuwa akiwafokea wachezaji wake pale walipofanya vibaya.

Mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo walionekana kumsifia kocha huyo, huku wengi wakiamini kuwa kama ataendelea hivyo, Yanga itakuwa bonge la timu.
Maximo aliongoza mazoezi hayo kwa ustadi wa hali ya juu, huku msaidizi wake naye akiwa moto kwenye kila kitu ikiwa ni pamoja na kukimbia, kupiga pasi na kukaba.

Hata hivyo, Coutinho kuna muda alidondoka na kuchubuka mguuni, lakini bado aliendelea kukipiga hali iliyowafanya mashabiki washangilia.

Mazoezi ya jioni yalikamilika saa 11:45 jioni na kukamilisha saa nne za Maximo za siku ya kwanza, huku Coutinho akifunga mabao mawili.

Wachezaji wa kikosi cha kwanza waliohudhuria mazoezi ya jana ni Juma Kaseja, Ally Mustapha ‘Barthez’, Juma Abdul, Salum Telela, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Omega Seme, Rajab Zahiri, Mbuyu Twite na  Saleh Abdallah pamoja na wa kikosi cha pili..
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mazoezi ya kwenye mchanga, watakaosa tb kweli hapo?

    ReplyDelete
  2. We c no cmba acha wapate tb hauakuhsu

    ReplyDelete
  3. huyo ndiyo MARCIO MAAXIMO banaaaa, msimbazi, mbeya city, lambalamba kaeeni chonjo saaannaaa!

    ReplyDelete

Top Post Ad