Ridhiwani Ataja 11 Wanaotosha Kugombea Urais 2015

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametaja majina 11 ya wanachama wa CCM wanaofaa kuwania urais kurithi kiti cha baba yake, Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake mwakani.

Ridhiwani (35), ambaye alishinda kiti cha ubunge wa Jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu, alitaja majina hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.

Miongoni mwa aliowataja kuwa wana sifa ni makada watano walio chini ya uangalizi wa CCM wa mwaka mmoja baada ya kubainika kuanza kampeni za urais mapema, mawaziri wawili waliopoteza nyadhifa zao katika kashfa ya Operesheni Tokomeza, mwanamke mmoja na Rais wa Zanzibar.

“Kutaja majina tu, naweza kuorodhesha wengi tu. Naweza kuorodhesha hata watu 500, kwa sababu tunaona wengi sana,” alisema mtoto huyo wa Rais Kikwete ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa muda mrefu akitokea umoja wa vijana wa chama hicho, UVCCM. “Kwa mfano, kwa upande wa Bara tunao Emmanuel Nchimbi, William Ngeleja, January Makamba, Bernard Membe, Steven Wassira, Edward Lowassa na Asha-Rose Migiro,” alisema.

Aliongeza: “Hawa ni kwa uchache zaidi… ni baadhi ya watu ambao wanatajwa kwa upande wa Bara, lakini jambo la msingi ni nani mwenye sifa za kuwa rais.”

Alisema pamoja na kwamba wanasiasa hao wote wanazo sifa za kuiwania nafasi hiyo ya juu, vikao vya chama ndivyo vitakuwa na nafasi ya kuwachuja ili kupata wanaotosha. “Kama wanatosha au la, vikao vya chama vitakaa kuamua licha ya kuwa hao wote niliowataja, kwa sifa za kugombea urais wote wanajitosheleza. Wana sifa, wana uwezo wa kugombea na wana uwezo wa kushinda, hao ni kwa upande wa Bara,” alisema.

Alipoulizwa hali ikoje kwa upande wa Zanzibar, Ridhiwani alisema, “Sisi chama chetu kina utajiri wa watu kwa upande wa Zanzibar kuna Shamsi Vuai Nahodha, Hussein Ali Mwinyi, Dk Seif Ally Iddi (Makamu wa pili wa Rais Zanzibar) na Dk Mohammed Ali Shein, Rais wa Zanzibar. Hawa ni watu ambao wana uwezo na hata wakipewa jukumu la kuongoza nchi hii wanaweza. Tunao wengi sana.”

Membe, Wassira, Lowassa, Ngeleja na Makamba walipewa adhabu na Kamati ya Maadili ya CCM ya kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama wala kufanya kampeni baada ya kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho, wakati Nchimbi na Nahodha walilazimika kujiuzulu nyadhifa zao za uwaziri kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza ambayo ililenga kushughulikia majangili, lakini ikahusishwa na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.

Ridhiwani hakumtaja Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye ambaye pia anatumikia adhabu hiyo ya Kamati ya Maadili ya CCM.

Quote of the Day
You are always a student, never a master. You have to keep moving forward.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbona umetaja wote mafisadi? Kiboko yenu Ni MAGUFULI, na nyie mafisadi wa ccm hamuwezi kumchagua JOHN MAGUFULI, kwani mnamfahamu Hana mchezo, atawapeleka nyote mafisadi WA ccm kunyea debe segerea! Na mnafaham angeanza na huyo Baba yako!

    ReplyDelete
  2. wanaofaa ni watu wa ccm tu eeeh!! dah hii nchi ishageuka ya watu fulani, hata kama unapendelea chama chako lakini kuwa transparent tu na useme hata wa upenzani, utaonekana unapoint

    ReplyDelete
  3. wote aliowataja hawafai mdau wa 10:16Am kwa taaaarifa yako ndugu ccccmmm!

    ReplyDelete
  4. Kawataja wanaofaa kulingana na mtazamo wake, na ww taja wako kwani unakatazwa jamani kuna watu huwa ni wazito kuelewa mada.

    ReplyDelete
  5. mbona kawataja mafisadi watupu?hatutaki kuongozwa na mafisadi wa richmond.

    ReplyDelete
  6. eti watu wanataka kumpa urais fisadi L,mnaakili kweli?

    ReplyDelete
  7. Umenifurahisha Sana mdau umeona wametaja mafisadi Tu! Na hicho chama kama cha ukoo vile!

    ReplyDelete
  8. Ametaja marais akiwa kama nani?

    ReplyDelete

Top Post Ad