Tudd Thomas ataja kiasi alicholipwa na Diamond na Ommy Dimpoz kufanya 'MdogoMdogo na Ndigushima'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtayarishaji wa muziki Tanzania Tudd Thomas ndiye aliyetayarisha wimbo wa Diamond ‘MdogoMdogo’ ambao unafanya vizuri sana  pamoja na wimbo wa Ommy Dimpoz ‘Ndagushima’ ambazo zote zimepata nafasi kubwa huku wasanii hao wakilipa mamilioni kufanya videos.

Akiongea katika kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm na Fadhili Haule, Tudd amesema kuwa alilipwa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kila wimbo katika nyakati tofauti.

“Kikawaida huwa wanasema sio vizuri kwa kuwa ni biashara lakini mimi niko real, ni two million kwa kila wimbo.” Alisema.

Ameeleza kuwa gharama za nyimbo hizo zilitokana na ukubwa wa nyimbo zenyewe na muda alioutumia kukaa studio na wasanii hao.

Tudd amesema wimbo wa ‘MdogoMdogo’ ulitengenezwa kwa muda wa miezi mitatu kwa kuwa ulikuwa wimbo mgumu kwao wote kwa kuwa ilikuwa idea mpya kwa wote, wakati wimbo wa Ommy Dimpoz ulimchukua miezi miwili kuukamilisha.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndiyo maana wao ni matajiri na wewe ni maskini tu. Wanakupa milioni mbili kuwafanyia kazi kwa kwa miezi miwili halafu wao wanakwenda kuitumia kazi hiyo kupata milllioni 10 kwa siku moja tu tena wanarudia rudia kwa muda mrefu hadi inawaingizia zaidi ya millioni mia moja! Mngejua jinsi maprodyusa wenzenzu kama wale wa Marekanei wanavokula bata msingekuwa mnakubali kutumiwa vile.

    ReplyDelete
  2. Nkajua kakulipa mil10, ujinga huo.

    ReplyDelete
  3. kaka milioni mbili ni ndogo sana, wanakunyonya hao, yani kumbe kuproduce huku ni cheap hv?

    ReplyDelete
  4. Huyu nae kumbe fala m 2 anaona peesa anakunja mgongo miezi mi3? Tutolee utaahira wako na utakufa maskini fxyuuuuu! !

    ReplyDelete
  5. kwendaaaaaaaaa yan

    ujaifikia ata shopping ya mbwa wa madam.

    ReplyDelete

Top Post Ad