UKATILI: Mtoto Afichwa Uvunguni kwa Miaka 6 Huko Morogoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakati jamii ikiwa bado haijasahau mateso aliyoyapata mtoto Nasra Mvungi na kusababisha  kifo chake, tukio lingine la aina hiyo limetokea katika Kijiji cha Matongola, Tarafa ya Magole Wilaya ya Kilosa, baada ya kubainika mtoto wa miaka sita akiwa amefichwa uvunguni mwa kitanda na kufanyiwa vitendo vya kikatili na mama yake mzazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa za mateso ya mtoto huyo zilifikishwa Kituo cha Polisi wilayani Kilosa  saa za mchana jana, baada ya uongozi wa  kijiji na kata kutoa taarifa na tayari mwanamke huyo amekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Mama aliyefanya ukatili huo anafahamika kwa jina la Sala Mazengo ambaye alimficha ndani mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Devota Malole na kumfanyia vitendo vya kikatili ikiwa pamoja na kutompa chakula, wala kumfanyia usafi.

Baada ya kufichuliwa kutoka alipofichwa, mtoto huyo alionekana kuwa dhaifu kiafya kutokana na kukosa lishe pamoja na mazingira aliyokuwa akiishi kutoridhisha, jambo ambalo ni kosa kisheria, pia ukiukwaji wa haki za watoto.

Inadaiwa kuwa tangu mwaka 2009 Sala amekuwa akimficha mtoto wake huyo ambaye sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kupatiwa vipimo na matibabu.

Hata hivyo, mwanamke huyo alipoulizwa alidai kuwa afya ya mtoto wake ilikuwa mbaya tangu alipozaliwa kutokana na magonjwa ya mara kwa mara, pia hali ngumu ya maisha ilichangia kudhoofisha afya ya mtoto huyo.

Alidai kuwa ana watoto sita, pia alikiri kumlaza chini mtoto huyo kutokana na kuwa na kitanda kimoja, ambacho hakiwatoshi watoto hao.

Aliongeza kuwa hata chakula amekuwa akikipata kwa shida kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa kuwa ana mtoto mwingine mdogo.

Kamanda Paulo alisema kuwa  mwili wa mtoto huyo umedhoofu kutokana na kufichwa ndani kwa muda mrefu na bado mwanamke huyo hajaeleza sababu za kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto huyo.

“Siwezi kutoa taarifa ya kidaktari, lakini kutokana na afya ya mtoto yule na mazingira tuliyomkuta ni dhahiri alikuwa akipata mateso na kufanyiwa vitendo vya ukatili. Hata hivyo, uchunguzi zaidi tunaufanya na kwamba taratibu za kumfikisha mtuhumiwa huyo Kituo Kikuu cha Polisi mkoani hapa zinaendelea,” alisema Kamanda Paulo.

Alisema kuwa mpaka sasa bado haijafahamika kama mtoto Davota ni mlemavu au la na kwamba taarifa za afya ya mtoto huyo zitatolewa baada ya madaktari kumfanyia uchunguzi wa kina.

Quote of The Day:
Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wanasema mama ndio anahuruma na mtoto wake.....jamani wapo wamama wanaroho mbaya adi kwa watoto wake..sijui ni kwann au ndio shida za dunia...ona sasa mama unamtesa mtoto wako kiasi hicho wala ukumbuki uchugu ulioupata wakati unamleta duniani..inauma sna sna

    ReplyDelete
  2. Du hy mama ni mchawi

    ReplyDelete
  3. WATOTO HAWA NI MISUKELE NA WANEFANYIWA MAZINGARA/DAWA ZA KISHIRIKINA HAWAWEZI KUISHI NJE YA MAZINGIRA HAYO WATAKUFA. MOROGORO YAPO SANA. WANAHARAKATI TUPAMBANE NE WACHAWI HAWATUSIJE NASI KUWA MISUKULE

    ReplyDelete
  4. tusitoe lawama kwanza kwa huyu mzazi kwadababu taarifa ya kwanza mzazi ameeleza mtt toka amezaliwa ana matatzo ya afya pili maisha magumu yamechangia hilo fikiria huyo mama ana watt 6! kuusu mtt kulala chini ameeleza kua anakitanda kimoja atafanyaje? huenda ikawa ilikua analala nae chini hapo uwezisema anamtesa. cha muhimu huyo mama nikusikilizwa kwa makini tu lkn co kukurupuka kumlaumu. l

    ReplyDelete
  5. We nae fala tu,una maisha magumu unazaa watoto sita wote was nini

    ReplyDelete
  6. Wee mdau unayetete huu ufirauni umefikiria kweli?? Hali mbaya watt 6 tena wengine Ni wadogo zaidi ya huyo anayemtesa! Labda ungesema huyo mwanamke Ana matatizo makubwa ya akili, kidogo ningekuelewa. Mungu mpe afya njema mtoto.

    ReplyDelete

Top Post Ad