Kauli ya Mwisho ya Ballali Kabla ya Kifo Chake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar na Marekani. Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania BOT), Marehemu Daudi Ballali aliacha wasia unaotaka maiti yake isionyeshwe hadharani atakapofariki dunia na wala maiti yake isiletwe Tanzania kwa ajili ya maziko.

Ballali aliyefariki Mei 16, 2008 na kuzikwa Mei 23 mwaka huohuo katika makaburi ya Gate of Heaven, eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani alifahamu kuhusu kifo chake wiki mbili kabla, baada ya matibabu kushindikana.

Mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa nchini Marekani kwa siku kumi kufuatilia suala hilo, alibaini kuwa kiongozi huyo alilazwa mara ya pili katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha George Washington, April 2008 na alirejea nyumbani kwake, Washington DC wiki mbili kabla ya kukutwa na mauti.

Habari kutoka ndani ya familia yake zinasema baada ya madaktari kushindwa kumtibu walimwambia kwamba asingeweza kuishi kwa zaidi ya wiki mbili, hivyo walimshauri ahamie kwenye ‘hospice’ ambayo ni nyumba maalumu ya kusubiri kifo kwa watu ambao magonjwa yao yameshindikana.

Hospice hutumika kwa ajili ya kuwaweka wagonjwa wanaohitaji faraja hasa kutoka na maumivu makali chini ya uangalizi wa washauri na wauguzi kwa lengo la kuwaongezea wagonjwa husika siku za kuishi.

Baadhi ya hospice hutoa huduma za kiroho, kijamii na kifedha na wakati mwingine huduma hizo hutolewa kwa wagonjwa ambao wanaugulia nyumbani. Hata hivyo, gazeti hili lilidokezwa kwamba Ballali alikataa kwenda kwenye nyumba hiyo na badala yake kutaka apelekwe nyumbani kwake.

“Alikataa kwenda kwenye hospice, aliwaambia madaktari kwamba yeye hawezi kwenda huko ijapokuwa kuna huduma nzuri na uangalizi wa nesi (muuguzi). Aliwaambia kwamba nitakwenda kufia nyumbani kwangu maana nina nyumbani kwangu,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Aliporejeshwa nyumbani, alikuwa anazungumza kama kawaida lakini kadri siku zilivyosogea hali ilikuwa ikibadilika na kama sikosei siku mbili au tatu za mwisho (za uhai wake) alikuwa anajitambua lakini alikata kauli, hakuwa akizungumza chochote”.

Uchunguzi wetu umebaini kuwa katika siku hizo za mwisho za uhai wake, Ballali aliacha maelekezo kwamba pindi atakapofariki dunia, mwili wake usiwekwe hadharani kwa maana ya kutazamwa na watu nje ya familia wala kusafirishwa kuja Tanzania kwa ajili ya maziko.

“He said, he doesn’t like to be turned into a laughing staff (alisema asingependa kugeuzwa kichekesho), sababu watu wasingekuja kutoa heshima za mwisho, bali wangekuja kumdhihaki kuangalia Ballali aliyetuhumiwa kwa ufisadi wa EPA na siyo Gavana,” kilisema chanzo hicho.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hamna kitu mnatufanya watanzania mabogus na habari zenu za kughusi .

    ReplyDelete
    Replies
    1. tupe khabari mdau. za kugushi kivipi?

      Delete
    2. Tugaie habari we ulishawahi muona nn baada ya kifo chake

      Delete
  2. Sasa jamani story za huyo Baba leo hii zimetokea wapi????....Huyo Baba aliishajiendea zake kimya kimya baada ya majungu na fitina nyingi za Watanzania. Sasa leo hii mnaleta story zake bila hata ya aibu. Mwacheni Mzee wa watu apumzike kwa amani. RIP Ballali.

    ReplyDelete
  3. Weka cheti Cha kifo.. Bado ninawasiwasi Huyu jamaa yupo akitafuna kodi zetu

    ReplyDelete
  4. Why this time and not that moment when he was needed most?! Watanzania nawaambia kuna movie nyingine inatengenezwa hapa.subirini mtaona mengi.hii ndio serikali ya Tanzania bana kugeuza watanzania wote ni mazezeta kwao ni kitu kidogo sana

    ReplyDelete
  5. duh Huyu jamaa bado nawasiwasi nae anaendeleaje kupiga msosi kama kawa

    ReplyDelete
  6. Ila kiukweli kama angekuwa hai hapo alipo hadi leo hajawahi kutuna ma mtz yeyote jamani siamini itakuwa alifariki bhana

    ReplyDelete
  7. huyu nakutana nae huku wajameni sema sasa kawa kama mzungu. kajibadillisha mno hamuwezi mtambua.

    ReplyDelete
  8. hakuna lolote hajafa yupo anakula bhata tu!

    ReplyDelete

Top Post Ad