Watangazaji watanzania mjifunze kutoka kwa Regina Mwalekwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwanza Hongera Kwa Kupata Kazi Mpya BBC
Yaani hakuna watu wananikera kusikiliza kama hawa vijana ambao wanajiita "wanavipaji" vya utangazaji na mbaya zaidi hawana taaluma ila wanaishi kwa kudra za Mungu tu.Ebu angalia ubunifu na weledi alionao Regina Mwalekwa kwenye utangazaji na hata ubunifu wa vipindi vyenye maudhui ya kuelimisha na si kukaraisha msikilizaji.

Leo hii mpaka nawashangaa TCRA kwa kushindwa kuchukua hatua kwenye radio za hawa watu ambao wanajiita ni radio ya watu kama vile radio zingine ni za mapaka vile.

Kipindi cha mida ya saa fulani za asubuhi mpaka muda wa maakuli,yaani hiki kipindi mimi ningekuwa nina mamlaka huko TCRA ningekifungia kabisa.

Sikatai kuna maswala wanazungumzaga yanagusa jamii ndio,lakini sio kipindi ambacho unaweza sema kina caliber ya ushindani katika tuzo za kimataifa na ndio maana wanakosa hata tuzo za TASWA sijui zile!

Mimi sio mwandishi lakini nadhani hakuna ethic inayomtaka mwanahabari kuongea mambo ya ajabu katika radio ya umma nkimaanisha inayosikilizwa na watu wengi na wa rika mbalimbali.. 

Yani radio hyo ya Mikocheni yenye vijana wanaovaa milegezo ndio watangazaji ambao maneno machafu midomoni mwao ni kama sala kitu ambacho kilimtofautisha sana dada Regina na vijana hawa,lakini pia kwakuwa Regina alitambua kuwa radio ya vijana wanahitaji kufahamu lugha adhimu ya kiswahili aliamua kuwa na segment ya angalau neno moja kila siku ili vijana waelewe walau matumizi ya maneno.

Ila la kheri Regina na kama hao mabinti na vijana wanaosema "wanavipaji" watashindwa kujiendeleza kielimu wakiendelea kubweteka kwakuwa bosi anawapa vocha na wanajulikana na vijana basi Mungu awasaidie lakini wataishia hapa hapa na hawatakaa wapate exposure katika maeneo mengine.
By Bomouwa Via JF
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kiukweli Regina alipwaya kwenye ile redio kabisaaa. Anyway kwa kuwa alikuwa likuwa na malengo hongera zake tena Sana. Nina imani Kuna kipindi alikita kujiunga nao

    ReplyDelete
  2. Tunasubiri kijana wetu Millard ayo kwa miaka ijayo kwani anakipaji cha ukweli

    ReplyDelete
  3. Mwandishi unachuki binafsi...we unazungumzia tuzo za taswa akati radio Ina tuzo za superbrand miaka mitatu mfululizo...

    ReplyDelete
  4. Na Regina yupo kwny kipindi cha tv jina sijalishika huko kwny radio mnapomzngumzia mmepotea na bora umesema cyo mwandishi maana ulichokiandika unaonyesha dhahiri upo upande gan?'

    ReplyDelete
  5. Una jadili ujinga mnasema radio ya watu wasiojielewa harafu unamtaja Regina unaona unajielewa,Radio ambayo haina hao labda ni radio 1 tu,Kaa ufuatilie kafuatilie watangzaj worldwide,utangazj cyo kuvaa kama mlokole tu maana ndicho unachofikiria,Salim kikeke mwnyw mpaka anatoa freestyle kwny BBC swahili'

    ReplyDelete
  6. acha unafiki Regina mwenyewe alikua redio ya watu!umekosa cha kusema huna jipyaaaah

    ReplyDelete
  7. A cha majungu.ukifata yasokuhusu utapata la kukukela

    ReplyDelete
  8. Unamajungu we mwandishi unataka wavaeje labda kaah ... c o mbaya ongela dada Regina

    ReplyDelete

Top Post Ad