Maajabu : Mke wa Mchungaji Ajifungua Hirizi Baada ya Ujauzito wa Miezi 9 huko Bagamoyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wazee wetu walishawahi kuneno kwamba; Ukishangaa ya Mussa utayaona ya filauni! Ndivyo unavyoweza kuanza kusema kuhusiana na tukio la kushangaza lililotokea Kijiji cha Udindila Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT aliyetambulika kwa jina la Boniface Onesmo alijikuta akibubujikwa na machozi mara baada ya kushuhudia mkewe Bi. Benta Boniface akijifungua hirizi baada ya kushika mimba kwa kipindi cha miezi saba na nusu!

Akizungumza na mtangazaji wa Kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Edson Mkisi Jr, Mchungaji huyo alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo mkewe amekuwa na matatizo ya kuharibika kwa mimba za mara kwa mara na tangu kuhamia kwa eneo hilo la Udingila Bagamoyo mkewe huyo hajawahi kuzaa mtoto hata mmoja angawa amekuwa akishika mimba kila walipohitaji kuzaa.

“Kwa hakika Mungu ni mwema na sitaacha kuendelea kumsifu na kumuabudu,” alianza kueleza Mchungaji Onesmo.

 “Zaidi ya mtoto huyu mmoja niliyemzaa kabla ya kuhamia hapa, hivi sasa kila ninapotaka kuzaa mtoto mimba za mke wangu zinaharibika na hadi muda huu mimba zaidi ya nne zimeshaharibika na hii nyingine ndio amezaa hirizi!” Mchungaji Onesmo alisimulia.

Aliezeza kuwa siku ya tukio, mkewe kipenzi alianza kusikia uchungu tangu saa nne asubuhi na kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo uchungu ulipozidi kuongezeka.
  
Hali iliendelea hivyo hadi saa nne usiku ambapo mkewe alihisi kabisa kupushi na mimi nilikuwa tayari kumsaidia lakini wakati anaendelea kupushi mkewangu akawa anatoa haja ndogo mara kwa mara na alitoa haja ndogo hadi ndoo nne ndogo zilijaa na kumwaga nje.

“Baada ya hapo aliendelea kusikia maumivu makali ya tumboni huku akihisi kuzaa lakini baadae aliposikia mtoto anakuja na mimi kujiweka tayari kumzalisha niliona kitu kinatoka kama mtoto kukivuta ikatoka hirisi ikiwa imefungwa kitambaa chenye rangi chekundu na nyeusi!” anasema.

Aidha, kwa upande wa mkewe, alisema kama siki hiyo kungekuwa na sumu ya panya angekunywa afe akapumzike.
Akizungumze huku akilia, mama Dotto (Benta), anasema siku ya tukio hilo roho yake ilinusa kaburi kama kama kungekuwa na hata mafuta ya taa kwenye kopo angekunywa ili afe.

Nilimuuliza mume wangu mara kadhaa kama kwenye kopo kuna mafuta ya taa lakini aliniambia yote aliweka kwenye kandiri (taa ya chemli) na hata nilipoangalia tunapoweka sumu sikuiona….kwa hakika kama ningekiona kimoja wapo ningekunywa nife! Nimetesema sana,” anasema mama Dotto.

Mama Dotto alisema pamoja na changamoto zote anazokutana nazo Bagamoyo lakini hajafikiria wala hafikirii kwenda kwa mganga wa kienyeji.

Siwezi kwenda kwa mganga wa kienyeji kwa sababu waganga ukienda wao huongeza tatizo kwa hiyo nitaendelea kumuomba Mungu hadi atakaposikia maombi yangu,” anasema huku akiangalia na mumewe pamoja na majirani waliofika kumjulia hali.

Akizungumza na Mkisi Jr, Mjumbe wa eneo hilo, Bw Hamza Adam, mbali na kuthibitisha kufahamu kutokea kwa tukio hilo, pia alibainisha kwamba mbali na tukio hilo ambalo hajawahi kukutana nalo tangu uhai wake, pia eneo hilo mifugo imekuwa ikifa hovyo bila kuwepo kwa ugonjwa wowote.

 Credit: Times Fm
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duu tanzania tumetisha! Kikwete ndugu zako hao wasaidie wamjue mungu!!

    ReplyDelete
  2. Mh wajuu umenichekesha huko ni uganga tu wakianguka mganga,yaani ni shiider

    ReplyDelete
  3. MUOMBE MUNGU MAMA DOTTO ATASIKIA KILIO CHAKO USIKATE TAMAA POLE SANA...

    ReplyDelete
  4. SIKILIZENI. SHUUDA NYININE NI ZA UONO. IVI KUNA BABA ANAEWEZA KUDAKA MAJI YA UCHUNU WA MKEWE WAKATI WA KUJIUNGUA. ACHENI KUUNGA SHUHUDA. SI RAHISI KUSUBIRI KUMZALISHA MKE WEWE MWENYEWE WAKATI UNAJUA MAMA ANAZAA KWA ATATIZO. HATA SISIS TUMEZAA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni uongo haswaaaaaaa,na hata waandishi nao ni mabwege,kwa nini wasiulize kadi ya clinic,au tuseme huko hanuna huduma za kiafya kiasi kwamba wanazalia majumbani?
      Kwendeni huko,Ni kama mnatafuta njia ya kupata pesa ya pole.tubuni.

      Delete
  5. Kweli uongo,mwandishi anasema mimba imekaa miezi 9
    mchungaji anasema mimba imekaa miezi 7 na nisu.
    Patamu hapoooooooooo

    ReplyDelete

Top Post Ad