Mauji ya Wanawake Arusha, Mama Fezza Kessy Nae Anusurika Kuuwawa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAKATI hofu ya mauaji ya wanawake ikiwa bado imetanda mkoani Arusha, mama mzazi wa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy ameponea chupuchupu baada ya kuvamiwa na majambazi wawili kisha kuporwa fedha.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jijini humo, Feza alisema mama yake aitwaye Rose Kessy alikutwa na masaibu hayo mchana wa saa nane, Jumatano iliyopita akiwa hatua chache kutoka nyumbani kwake, eneo la Boma ya Siara, Moshono.

“Watu wawili wakiwa na pikipiki walimsimamisha akiwa garini anarejea nyumbani, wakamteremsha na kuanza kumsachi, wakachukua pochi yake ambayo ilikuwa na shilingi laki tatu ndani. Wakati wanafanya tukio hilo watu walikuwa wanatazama tu bila kufanya lolote.

“Watu wengine walipita na gari wakataka kusimama, lakini wakaonyeshwa bastola na kupewa ishara ya kuendelea na safari. Yaani walikuwa wanafanya wakiwa hawana wasiwasi utafikiri ni askari vile, hivi hapa ndiyo nimerudi kutoka polisi,” alisema mshiriki huyo ambaye pia aliwahi kushiriki shindano la Miss Tanzania miaka ya nyuma.
GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukitaka kujua nchi hii ni uozo ndio mambo kamahaya,ngoja afe police au auwawe mkubwa mmoja ni ubinafsi tu hovyooo

    ReplyDelete

Top Post Ad