Mpambano Unaendelea Wema Sepetu Awatunza Fedha Chafu Yamoto Band

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

“MADAM…Madam…Madam…” ndizo kelele zilizosikika wakati Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ alipokuwa akimtunza fedha nyingi dogo machachari wa Bendi ya Yamoto, Asilahi Isiyaka ‘Dogo Aslay’.

Tukio hilo limetokea ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem na kuweka historia kwa Wema kuwa staa wa kwanza ‘kumwaga’ fedha wakati wa uzinduzi wa bendi ya Yamoto.

MAMBO YALIVYOANZA
Awali, wakati bendi ya Yamoto ilipokuwa ikitumbuiza, ulifika wakati kiongozi wa bendi hiyo, Said Fella alitambulisha uwepo wa Wema kwa kudai amemuwakilisha bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivyo apande jukwaani na kusema chochote lakini mrembo huyo akasema kilichompeleka ukumbini hapo ni uzinduzi wa Yamoto Band.

“Jamani nimekuja hapa kwenye uzinduzi wa Bendi ya Yamoto na siyo kumuwakilisha Diamond, ya huku hayamuhusu kabisa sasa semeni niwaimbie wimbo gani,” alisikika Wema Sepetu na kuanza kuimba wimbo wa Niseme ambao mashabiki waliupendekeza.

AMWAGA FEDHA
Mrembo huyo asiyechuja tangu alipotwaa taji la u-miss Tanzania (2006), akiwa na wapambe wake, baada ya kuimba kidogo, alichukua pochi yake na kuanza kummwagia fedha mfululizo Dogo Aslay huku akiwa anamzunguka kwa kucheza.

ASLAY APAGAWA
Kwa fedha hizo zilizokadiriwa kuzidi milioni moja alizotunzwa Aslay, ilifika wakati dogo huyo akawa anaziangalia tu kama bubu na kupigwa butwaa huku akiishia kuzitazama bila kuimba chochote.

BAUNSA AMZUIA WEMA
Katika hali iliyowashangaza wengi, baunsa mmoja aliyekuwa akimlinda Wema alimzuia staa huyo kuendelea kutoa fedha zaidi akidai zimetosha ndipo akaacha na kushuka jukwaani.

KWA NINI ASLAY TU?
Wakati zoezi hilo likiendelea, kuna baadhi ya mashabiki waliibua minong’ono wakihoji kwa nini atunzwe Aslay peke yake wakati bendi hiyo ina wakali wengine watatu, Malomboso, Enock na Beka?
“Mbona kama anampendelea Aslay tu  wengine hawatunzi ona hela zote ameshikilia yeye tu kweli, inaonekana anamzimia sana Aslay, si bure, haikatazwi lakini,” alihoji shabiki mmoja aliyekuwa akifuatilia shoo hiyo.

MPAMBANO UNAENDELEA!
Wema ameonekana kuja juu kwa sasa kifedha, wiki iliyopita alifanya tukio kama hilo katika Ukumbi wa Thai Village Masaki kwa kumtunza ‘pesa ndefu’ mwanamuziki wa Bendi ya Skylight, Sam Mapenzi huku ikidaiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kumziba mdomo aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ambaye inadaiwa kwa sasa yuko ‘vizuri’ kifedha.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HIYO ELA ANGEITUMIA KUFUNGUA BIASHARA YAKUMSAIDIA SIFA ZA KIJINGA MJINI ZINAMPONZA

    ReplyDelete
  2. tupeni ubuyu wa insta basi jamaniii eeehh kinaendaje wema na chibu dangote tunataka sherekea birthday wiki hii sie aarrrghh!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hasa zawadi itakuwa...............................?

      Delete
  3. Upedejee haupendezi kwa mwanamke

    ReplyDelete
  4. hahaha sherehe ipo lkn wema hana shida na diamond mana ameona anamfaidisha tuuu na yy anakosa pesa ..amemsaidia mpaka kuongea kidhungu alikua teeeeh....sasa wema anarud kwa aslay..kwa kas diamond atajuutaa kwanza aslay ndo itakua couple ya kufa mtu mana angalau anaonekana kua kijana mmh diamond hamna kitu

    ReplyDelete
  5. Kweli Wema sikio la kufa.
    Umri unaenda mamy

    ReplyDelete
  6. Ni shidaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa?????

    ReplyDelete
  7. mi hizi story sitaki kuziamini mpaka birthday ya madame na chibu ipite ndo niami, madame ananikera tabia yake ata nikafikiria chibu asipomuoa poa tu ila leo niliposikia ubuyu wa insta kama wameachana karoho kangu hakakufurai ata kidogo ata nawish iwe urongo tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna kuachana,sie twasubiri wedding
      ya kufanyika uwanja wa Taifa.

      Delete
  8. umependeza wema,sasa endelea kumuendekeza huyo domo wako,akuzeeshe tena,muongo huyo akiona unapendeza anakuacha,yeye anataka mwanamke akiwa naye yeye basi,at a kuoga asioge,penny alikuwa hivyo hivyo alimfuja weee,penny kaondoka anapendeza sasa hivi,mwache akamuoe huyo mennina na hivi bado mdogo atajuta ,hakuna mume hapo,ushamba mwingi,kwanza mimi nimemuona domo mshamba,kapost ratiba ndefu ya show zake huko nje ya nchi,kumbe hajalipwa,hana mkataba na huyo promota,ili mradi tu kutaka kumrusha roho kiba,aonekane ana show nyingi nje,kumbe,ujinga mtupu,wenzie kina davido na tiwa,wametumbuiza kesho wamerudi kwao,yeye na ushamba wake,kakalia kutafuta show za uchochoroni,hovyo,

    ReplyDelete
  9. domoooo ana shidaaaaaaaa!! ndiyo maanaaaa anakurukupuka kusaka shooos feki, kumbe demu yake mburula hvi!! anamwaga pesa zake tu!!

    ReplyDelete
  10. MDAU HAPO JUU UNASEMA NINI?ATI?MENINA SI ALIAPA MIUNGU YOOOOTE DUNIANI KWAMBA HAJAWAHI MVULIA CHUPI DIAMOND?JOHARI NAE ANADAI ETI HAJAMVULIA CHUPI RAY,HIVI HAWA WATU KWANINI WANAFANYA WATU KAMA WATOTO WADOGO VILE.MENINA PALE ANAFUATA KITU SIO SURA YA DIAMOND.DIAMOND WENZIO WANAKUPENDA KWAKUWA UNA JINA UKIFIFIA WANAKUTUPA KULE MALI ULIZOCHUMA MNAGAWANA NA MKEO MENINA NUSU KWA NUSU.

    ReplyDelete
  11. WEMA WE NI SIKIO LA KUFA HATA ULITIE DAWA VIPI ALISIKII,WE WAKURUDIANA NA DOMO KWELI?HAYA MOVIE IMEISHA SASA.TUNASUBIRI BIRTHDAY YAKO.

    ReplyDelete
  12. ubuyu wa inst nimeupenda.................tena staki wema akae na domo domo sio mwanaume kwanza hana hata sura ya kiume yupo km maiti vile staki kusikia wema anamlilia domo domo hamna kitu wema madam nenda kwa aslay ndo mwanaume....anaonekana hata ukitoka nae jaman

    ReplyDelete
  13. lol watuz ati aslay basi uyo wema atakuwa mgojwa kisa na kutoka na vitoto vidogo ata havijakua nini? madame hawezi toka na vitoto coz ni MVIVU akitoka na mtu lazima awenazo ndefu mana ndo keshaamua kufanya papuchi mtaji, diamond wa watu akasake mavumba uko halali kila siku yuko angani anakaribia kupigwa viti vya uso alete nyumbani ale na familia yake kisha wengine wakagawe ivi ivi kwenye viwanja vya starehe na huku group la wapambe basi nae mgojwa itakuwa uyo dai ila yote kabisa kama dai kambwaga kwa tabia big up ila kama kwa umalaya wake yatamkuta tu nae mda si mrefu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chaz baba alishakuwa na hela ndefu gani?malaya tu madame.

      Delete
  14. DOMO YATAMKUTA TENA SI MADOGO

    ReplyDelete

Top Post Ad